NAIBU WAZIRI WA KAZI NA AJIRA AFUNGUA SEMINA YA VIJANA MKOANI LINDI

Posted in
No comments
Tuesday, February 24, 2015 By danielmjema.blogspot.com

Mgeni rasmi kwenye mafunzo ya stadi za kazi na utambuzi wa fursa za kiuchumi zilizopo mkoa wa Lindi Naibu waziri wa kazi na ajira mhe.Dr. Makongo Mahanga (MB) amewataka vijana wa mkoa wa Lindi kuyageuza mafunzo watakayoyapata ya stadi za maisha sanjari na kuzitambua fursa zilizopo ndani ya mkoa, waweze kujiajiri na kujikomboa kiuchumi,wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo ambapo jumla ya vijana 360 kutoka halmashauri sita zilizopo mkoani Lindi wameudhuria kwenye ukumbi wa kanisa katoliki Mt.Kagwa. Vijana 360 kutoka kwenye wilaya za Kilwa, Ruangwa, Liwale, Nachingwea, Lindi Mjini na Vijijini ambao ni washiriki wa mafunzo wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi naibu waziri wa kazi na ajira Mhe.Dr.Mkaongoro Mahanga hayupo pichani.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Mwantumu Mahiza akiwaeleza washiriki wa mafunzo ya stadi za maisha sambamba na kufahamu fursa za kiuchumu ambapo mpango wa kuendesha mafunzo hayo umebuniwa na yeye mwenyewe,mbele ya mgeni rasmi, wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Baadhi ya wakuu wa taasisi mbalimbali wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe.Mwantumu Mahiza alipokuwa akijadiliana nao kuhusu umuhimu wa kuwapa elimu ya ufahamu wa mambo yanayotekelezwa na taasisi hizo mkoani lindi,kulia ni meneja wa shirika la nyumba bwn.M.Peter,anayefuata meneja wa CRDB(PLC) na mwenye miwani katikati ni Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi Fortunata Kullaya.
Katibu tawala wa mkoa wa Lindi Ndg. Abdlla Chikot akijadiliana jambo na wakuu wa wilaya ya Kilwa kushoto mhe.Abdallah H. Ulega,kulia ni Mkuu wa wilaya ya Liwale mhe. Ephrem Mmbaga,nje ya ukumbi wa mafunzo wa Mt. Kagwa Lindi.
Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi Fortunata Raymond akitoa taarifa ya madhumuni ya ofisi ya mfuko kushiriki kwenye mafunzo hayo kwa waandishi wa habari,ambapo elimu ya faida na umuhimu wa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii. (CHF) itatolewa hapo kesho kwa washiriki vijana.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .