NYALANDU AWAAGA WAFANYABIASHARA WANAOENDA KUSHIRIKI MAONYESHO YA ITB, BERLIN UJERUMANI
Posted in
Matukio
No comments
Wednesday, March 4, 2015
By
danielmjema.blogspot.com
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akitoa nasaha za kuwaaga wafanyabiashara wa Tanzania wanaoenda Berlin, Ujerumani kushiriki maonyesho makubwa Duniani ya biashara maarufu kama ITB kuanzia Machi 4-8 mwaka huu.(Picha zote na modewjiblog)
Na Andrew Chale wa modewji blog
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu amewataka wafanyabiashara wa Tanzania wanaoenda kushiriki maonyesho makubwa Duniani ya biashara maarufu kama ITB, mjini Berlin, Ujerumani Machi 4 hadi 8, mwaka huu, kubeba uzalendo na kuitangaza Tanzania hususani vivutio vya Utalii na utajiri wa maliasili ili kuvutia wawekezaji.
Nyalandu aliyasema hayo usiku wa Februari 27, wakati wa halfa fupi ya kuwaaga wafanyabiashara hao ambapo alisema kuwa, kwenda kwao huko kushiriki maonyesho hayo makubwa kabisa duniani, ni fursa kama Tanzania kupata kujitangaza zaidi na kuvutia wawekezaji.
Deputy Head of Mission wa Ubalozi wa Ujerumani, John Reyels akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.
“Leo hii tunawaaga hapa. Nyie ndio Tanzania hivyo mnapokuwa huko mjue mmebeba watanzania wengine zaidi ya Milioni 40. Ni wakati wa kuvitangaza vivutio na uzuri wa Tanzania na ilikuongeza soko letu la Utalii na uwekezaji” alieleza Nyalandu.
Pia aliongeza kuwa, Wizara yake ya Utalii itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha Taifa la Tanzania linafikia malengo yake yaliyokusudiwa ikiwemo kujitangaza ndani na nje ikiwemo kuendelea kuunga mkono juhudi za kupambana na Uharamia dhidi ya meno ya Tembo, wanyama na nyara za serikali kiwemo pembe za ndovu.
Afisa wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devota Mdachi (kushoto) akiwa na Dorothy Masawe (Kulia) kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, wakifuatilia jambo kwa makini wakati wa halfa hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu akibdilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa.
Deputy Head of Mission wa Ubalozi wa Ujerumani, John Reyels (kulia), Afisa wa Ubalozi wa Ujerumani kitengo cha habari, John Meirikion (kushoto) wakiteta jambo na mmoja wa wageni waalikwa.
CEO wa DHL ukanda wa Eastern Africa, Pramod Bagalwadi, akisalimiana na Waziri Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa ambao ni wafanyabiashara katika sekta utalii wakibadilishana mawazo kwenye hafla hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu katika picha ya pamoja na Afisa wa Ubalozi wa Ujerumani kitengo cha habari, John Meirikion wakati wa hafla hiyo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mh. Lazaro Nyalandu katika picha ya pamoja na wafanyabiashara akiwemo Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Bw. Florenso Kirambata ( wa pili kushoto).
Mkurugenzi wa Biashara wa Flight Link, Bw. Ibrahim Bukenya akiwa na Deputy Head of Mission wa Ubalozi wa Ujerumani, John Reyels wakati wa hafla hiyo.
Wadau wakifurahi jambo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :