Kuza uwekezaji katika kawi ya Afrika kwa ajili ya ushindi mara tatu kwa watu, kawi na sayari, ripoti ya Annan inahimiza
Posted in
Habari na Jicho Pevu la Kijiwe
No comments
Monday, June 8, 2015
By
danielmjema.blogspot.com
CAPE-TOWN, South-Africa, June 5, 2015/ -- Serikali
za Afrika, wawekezaji, na taasisi za kimataifa za kifedha lazima
zizidishe uwekezaji wao katika kawi ili kufungua uwezo wa Afrika kama
dola kuu la kiulimwengu la kiwango cha chini cha kaboni.
Huu
ndio ujumbe mkuu wa ripoti mpya kutoka kwa kundi la Maendeleo ya Afrika
ya Kofi Annan, Kawi,watu, sayari : Kutwaa nafasi za Kawi na Hali ya
hewa ya Afrika. Ripoti yenyewe inatoa mwito wa kuzidishwa kwa uzalishaji
wa kawi mara kumi ili kuwezesha Waafrika wote kupata umeme kufikia
2030. Hii itaondoa umaskini na ukosefu wa usawa, itaongeza ukuaji, na
kuleta uongozi wa hali ya hewa ambao unakosekana katika kiwango cha
kimataifa.
Ili kupakua nakala ya Ripoti ya Maendeleo ya Afrika ya 2015 tembelea www.africaprogresspanel.org.
Livestream of the event: http://www.weforum.org/events/ world-economic-forum-africa- 2015/player?p=1&pi=1&a=67597
“Tunapinga
kwa dhati wazo la kwamba Afrika lazima ichague baina ya ukuaji na
ukuzaji wenye kiwango cha chini cha dkaboni,” alisema Kofi Annan,
mwenyekiti wa kundi la maendeleo la Afrika. “Afrika yahitaji kutumia
nyenzo zake zote za kawi katika kipindi kifupi kijacho, huku ikijenga
misingi yenye ushindani ya miundo msingi ya kawi ya kaboni ya kiwango
cha chini.”
Katika
mataifa ya Afrika yaliyo chini ya Sahara, watu milioni 621 wanakosa
kufikia umeme – na idadi hii inaongezeka. Pasipo kuhesabu Afrika Kusini,
ambayo huzalisha nusu ya umeme wa sehemu hiyo, Afrika iliyo chini ya
Sahara hutumia umeme kiasi kidogo kuliko Spain. Itamchukua Mtanzania wa
kawaida wastani wa miaka minane ili kutumia kiasi sawa cha umeme na kile
Mmarekani wa kawaida hutumia kwa mwezi mmoja.Na katika kipindi cha
mwaka mmoja wa mtu kuchemshia birika mara mbili kwa siku nchini
Uingereza hutumia umeme mara tano zaidi kuliko vile Methiopia hutumia
katika mwaka huo huo.
Ukosefu
wa kawi hulemaza ukuaji wa eneo hili kwa asilimia 2-4 kwa mwaka,
ikirudisha nyuma juhudi za kutengeneza nafasi za kazi na kupunguza
umasikini. Kando na miaka kumi ya ukuaji, pengo la uzalishaji wa kawi
baina ya Afrika na maeneo mengine linazidi kupanuka. Nijeria ni dola kuu
inayouza mafuta nje ya nchi, lakini raia wake milioni 95 hutegemea
kuni, makaa na nyasi kama kawi.
Ripoti
yenyewe inadhihirisha kwamba nyumba zinazoishi kwa chini ya Dola $2.50
za Marekani kwa siku kwa jumla hutumia Dola bilioni $10 za Marekani kila
mwaka kwa bidhaa zenye uhusiano na kawi, kama vile makaa, mafuta taa,
misumaa na kurunzi. Ikipimwa kwa misingi ya kwa-kiasi , nyumba masikini
zaidi za Afrika hutumia yapata Dola za Marekani $10/kWh kwa mwangaza
mara 20 zaidi ya nyumba tajiri za Afrika. Kwa kulinganisha, gharama ya
wastani ya kitaifa ya umeme inchini Marekani ni Dola za Marekani
$0.12/kWh na Uingereza ni Dola za Marekani $0.15/kWh. Huu ni mwanguko wa
kiwango fulani cha soko.
Teknolojia
za ufanywaji upya wa gharama za chini zinaweza kupunguza gharama za
kawi, ikifaidi mamilioni ya nyumba masikini, kuleta nafasi za uwekezaji,
na kupunguza uchafu wa kaboni.
Ripoti
yenyewe inasema viongozi wa Afrika lazima waanzishe mageuzi ya kawi
ambayo yataunganisha wale hawajaunganishwa, na inayoshughulikia mahitaji
ya watumizi, biashara, na wawekezaji kwa ajili ya umeme wa gharama ya
chini na unaoweza kutegemewa.
Ripoti hiyo ya Maendeleo ya Afrika ya 2015 inahimiza serikali za Afrika :
•
Kutumia gesi ya asili ya eneo hilo kutengeneza kawi ya kutumika
nyumbani na pia kuuza nje ya nchi, huku ikikusanya uwezo mkubwa wa kawi
yenye kufanywa upya ya Afrika ambayo haijatumika.
•
Kusitisha ufisadi, kufanya usimamizi wa huduma kuwa wazi zaidi,
kuimarisha sheria, na kuongeza bajeti ya miundo msingi ya kawi.
•
Kuelekeza upya zile Dola bilioni $21 za Marekani zinazotumika kufidia
huduma zinazopata hasara na matumizi ya umeme– ambazo hufaidi haswa
matajiri – kuelekea fidia za uunganishwaji na uwekezaji wa kawi yenye
kufanywa upya ambayo huleta kawi kwa masikini.
Ripoti
hii inaomba kuimarishwa kwa uhusiano wa kimataifa kufunga pengo la
ufadhili wa sekta ya kawi ya Afrika, yenye kukadiriwa kuwa Dola bilioni
$55 za Marekani kwa mwaka hadi 2030, ambalo linajumuisha Dola bilioni
$35 za Marekani za uwekezaji wa viwanda, upeperushaji na usambazaji, na
Dola bilioni $20 za Marekani kwa gharama za ufikiaji kwa wote.
Hazina
ya kiulimwengu ya uunganishaji yenye lengo la kuwafikia Waafrika
milioni 600 zaidi kufikia 2030 inahitajika kuendeleza uwekezaji ndani na
nje ya mfumo wa ugavi wa kawi.
Wenye
kutoa msaada na taasisi za kifedha zinafaa kufanya kazi zaidi ili
kufungulia uwekezaji wa kibinafsi kupitia kwa dhamana na fedha za
kushughulikia madai.
Wakati wa kukomesha ‘mchezo wa shere wa mapatano ya hali ya hewa’
Ripoti
hii inatia changamoto serikali za Afrika na washirika wao wa kimataifa
kuinua kiwango cha malengo katika kongamano muhimu kule Paris mwezi
Desemba, na kuitisha mageuzi kamili kwenye mfumo wa ufadhili wa hali ya
hewa ulio katika vipande vipande, uliopungukiwa na nyenzo na ulioshindwa
kufanya kazi.
Madola
ya G20 yanafaa kutengeneza ratiba ya kuondoa ufadhili wa kawi ya
mafuta, ripoti yenyewe inaeleza, na kupiga marufuku ufadhili wa
utafutaji na uzalishaji kufikia 2018. “Mataifa mengi tajiri hutuambia
yanataka mapatano ya hali ya hewa. Lakini wakati huo huo mabilioni ya
madola ya pesa za walipa-ushuru zinafadhili uvumbuzi wa hazina mpya za
Makaa ya mawe, matufa na gesi,” Bw. Annan alisema.“Wanafaa kuwa
wakilipisha kaboni kutoka kwenye soko kupitia kutoza ushuru, sio kufidia
janga la hali ya hewa.”
Huku
tukitambua fanaka za hivi majuzi katika mapatano kuhusu nafasi za Umoja
wa Ulaya, Marekani na Uchina, ripoti yenyewe inasema kwamba mapendekezo
ya wakati huu yangali chini ya mapatano yanayoweza kuaminika ya kuwekea
mipaka ongezeko la joto duniani kwa kiwango kisichozidi 2˚C zaidi ya
viwango vya kabla ya wakati wa viwanda. Inashutumu Australia, Kanada,
Japani na Urusi kwa kujiondoa kutoka kwa mazungumzo yenye kufaidi na
kuhusisha wote kuhusu hali ya hewa.
“Kwa
kushikilia bahatisho zao na kungoja wengine wapige hatua kwanza, baadhi
ya serikali zinacheza shere na sayari na maisha ya usoni ya vizazi. Huu
sio wakati wa kudanganya, manufaa ya kibinafsi ya muda mfupi, na
malengo yaliyosongeka, lakini wa uongozi wa kiulimwengu wenye ujasiri na
matendo yenye maamuzi,” Bw. Annan alisema.
Bw.
Annan aliongezea, “Mataifa kama Ethiopia, Kenya, Rwanda na Afrika
Kusini yamejitokeza kama wenye kuongoza katika mabadiliko ya kiulimwengu
kuelekea kwenye kawi ya kanoni ya kiwango cha chini.. Afrika ipo kwenye
nafasi nzuri kupanua uzalishaji wa kawi inayohitajika kuendeleza
ukuaji, kutoa kawi kwa wote na kuchukua nafasi ya uongozi katika
mapatano muhimu ya mabadiliko ya hali ya hewa.”
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :