MDAHALO WA WAGOMBEA URAIS WA CCM ULIVYOYEYUKA NA KUHUDHURIWA NA MGOMBEA MMOJA AMINA SALUM ALI
Posted in
Habari na Jicho Pevu la Kijiwe
No comments
Wednesday, June 10, 2015
By
danielmjema.blogspot.com
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amina Salum Ali (kulia), akizungumza na wadau mbalimbali waliofika kwa lengo la kuwasikiliza wagombea hao ambao hawakufika.
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Amina Salum Ali, akitoka ukumbini katika Hoteli ya Hyatt Recency Kilimanjaro baada ya kuahirishwa kwa Mdahalo wa waliotangaza nia ya kugombea urais kupitia chama hicho kushindwa kuhudhuria Dar es Salaam juzi. Wagombea hao walioshindwa kuhudhuria mdahalo huo ni Mwigulu Nchemba, Samuel Sitta, January Makamba, Lazaro Nyalandu na Frederick Sumaye.
Dotto Mwaibale
WATANGAZA nia watano wa kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), waliokuwa wahudhurie mdahalo ulioandaliwa na Umoja wa Maofisa Watendaji Wakuu (CEOrt), walishindwa kuhudhuria mdahalo huo bila ya kuwa na sababu za msingi ambapo mgombea pekee Amina Salum Ali ndiye aliyejitokeza.
Wagombea walioshindwa kuhudhuria mdahalo huo wametajwa kuwa ni Samuel Sitta, Mwigulu Nchemba, Lazaro Nyalandu, Frederick Sumaye na January Makamba.
Mdahalo huo ulikuwa uonyeshwe moja moja na Kituo cha Televisheni cha Azam na Clouds TV ulihudhuriwa na watu mbalimbali na maandalizi yake yalikuwa yamekamilika.
Kuharishwa kwa mdahalo huo kuliwasikitisha wadau mbalimbali waliokuwa wamefika kushiriki wakisema kwamba wagombea hao hawakupaswa kufanya hivyo ukizingatia kuwa wote ni kutoka chama kimoja cha CCM.
Akizungumzia kuahirisha mdahalo huo, Mwenyekiti wa Mdahalo huo Ali Mafuruki hawakupata maelezo yoyote kutoka kwa wagombea ya kuto hudhuria.
Mtangaza nia pekee aliyefika kwenye mdahalo huo uliokuwa ufanyike ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro, Amina Salum Ali alisema amesitika sana kwa wenzake kwa kutofika.
Alisema midahalo kama hiyo ni ya muhimu na ina afya hasa katika wakati huu wa mchakato wa uchaguzi wa viongozi ambapo wagembea hawapaswa kutukanana bali kuelewana na kila mmoja wao kuzungumza kile anacho kiamini kwa maslahi ya taifa.
"Midahalo kama hii ilikuwa ni fursa kwa watangania kwani wananchi walitaka kujua tofauti kati ya mgombea huyu au yule lakini ndio hivyo wenzangu hawajakuja najisikia vibaya" alisema Ali.
Alisema anashukuru kupata uwanja wa kujiunga na wenzake hasa vijana katika kinyang'anyiro hicho ingawa amewatangulia kufanya kazi na kuyafahamu mambo mengi.
Ali alisema kwamba katika suala la kuinua uchumi haiwezekani kufanya jambo hilo kwa haraka ni vizuri kwanza vitu vikaweka sawa na kuwe na sera za kuweza kushawishi kwani hivi sasa kila jambo linakwenda kwa utaratibu.
Alisema yeye anafahamika sana na amefanyakazi Zanzibar na nje ya nchi na anauzoefu mkubwa ndio maana akaona anaweza kuongoza taifa iwapo jina lake litapitishwa kugombea nafasi hiyo.
Alisema kiongozi anayehitajika ni yule ambaye anaweza kusimamia kwa moyo wa dhati masuala ya gesi na uwekezaji katika maeneo mbalimbali ambapo yeye anaweza kutokana na uzoefu wake kwani anajua sheria na sera.
Watangania hao walioshindwa kuhudhuria mdahali huo baadhi yao walisema wameshindwa kufika baada ya kukosa nafasi kutokana na kuwa katika mchakato wa kwenda mikoani kutafuta wadhamini wa kuwajazia fomu za kugombea nafasi hiyo na wakaahidi wapo tayari kuhudhuria mdahalo utakaoandaliwa wakati mwingine. (Imeandaliwa na mtandao wa www. habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :