KENYA: MTU MMOJA AWAPA SUMU WANAWE HUKU NAYE AKIJARIBU KUJIUA.

No comments
Sunday, February 28, 2016 By danielmjema.blogspot.com

MKAZI mmoja wa eneo la Lumakanda, mjini Lugari, katika kaunti ya Kakamega, anadaiwa kuwaua wanawe wawili, wenye umri wa miaka miwili na 10, baada ya kuwanywesha sumu watoto wake wanne, huku naye akijaribu kujiua.




Kwa mujibu wa taarifa kutoka katika eneo hilo, mtu huyo kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya rufaa ya Moi Teaching, mjini Eldoret ambako anaendelea na matibabu kufuatia jaribio la kujitia kitanzi mara baada ya kuwaua watoto wake wa kuwaza kugonga mwamba.


Akithibisha tukio hilo, Chifu wa eneo hilo, Johana Kisoria, alisema kuwa watoto wengine wawili wamelazwa katika Hospitali ya Lumakanda, mjini Lugari ambako wanaendelea vizuri baada ya kunywa sumu hiyo. Inadaiwa kuwa mtuhumiwa huyo alichukua hatua hiyo baada ya kukimbiwa na mke wake.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .