KENYA: KUPPET YAWATAKA WALIOIBA PESA ZA NYS KUZIRUDISHA.
Posted in
afrika mashariki
No comments
Sunday, February 28, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Mwenyekiti
wa Chama cha walimu wa elimu ya ya shule ya msingi nchini Kenya, (Kenya Union
of Post primary Education Teachers), KUPPET, Omboko Milemba, watuhumiwa wote wa
sakata la wizi wa fedha za NYS, kurudissha pesa hizo.
Akizungumza
katika kaunti ya Busia, wakati wa Uchaguzi wa matawi wa Chama hicho, Milemba alisema fedha zilizoibiwa,
zikipatikana zitumike katika kuimarisha maendeleo ya walimu na kuhakikisha kuwa
makubaliano ya kuongeza mshahara kwa asilimia 50-60, inatekelezwa.
Alihatarisha
kuwa endapo Serikali itashindwa kuwatimizia matakwa yao, Walimu nchi nzima
wanaweza kulazimika kutoipigia kura serikali ya Jubilee katika uchaguzi mkuu,
unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Maigizo
yanayojitokeza katika sakata la uchotwaji wa mamilioni ya fedha ndani ya NYS, yanaendelea
kuzua hisia mbalimbali miongoni mwa wakenya huku Utumishi wa umma ukimtaka Rais
Uhuru Kenyatta na makamu wake, William Ruto, kuongoza harakati za kubaini wezi
wa fedha hizo.
Katika hati
ya kiapo iliyosomwa mahakamani, Waiguru anadai kuwa aliarifiwa na aliyekuwa
kaimu Mkurugenzi mtendaji wa NYS, Adan Harakhe, kuhusu madai ya mmoja wa
watuhumiwa, Ben Gethi, kuwa malipo feki yanayofikia Ksh800 million, yalifanyika
kwa ajili ya makampuni, yenye uhusiano na Waziri wa Uchumi, Henry Rotich ambaye
anadaiwa kuwa ni mpambe wa Naibu wa Rais, Wllium Ruto.
Waiguru pia
katika hati hiyo, amewahusisha watu wa karibu na Ruto, katika sakata hilo,
akiwemo msaidizi wa Ruto, Farouk Kibet, Sineta Kipchumba Murkomen na kiongozi
wa wajumbe walio wengi bungeni, Aden Duale.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :