RAILA: DUALE, MURKOMEN NA ROTICH LAZIMA WAWAJIBIKE!
Posted in
afrika mashariki
No comments
Sunday, February 28, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
KUFUATIA hatua
ya aliyekuwa Waziri wa Ugatuzi, Anne Waiguru, kuwatuhumu wanasiasa maarufu katika
muungano wa Jubilee, unaoongozwa Rais Uhuru Kenyatta, katika hati yake ya kiapo,
kuwa ni miongoni mwa waliohusika na sakata la uchotaji wa fedha katika Taasisi
ya huduma kwa vijana, National Youth Service (NYS), Waziri mkuu wa zamani, Raila
Odinga amewataka wote waliotajwa kuwajibika!
Raila
amewataka, Waziri wa Uchumi, Henry Rotich, kiongozi wa wajumbe waliowengi
bungeni, Aden Duale na kiongozi wa wajumbe waliowengi katika bunge la Senate, Kipchumba
Murkomen, kuwajibika kwa kujiuzulu kutoka katika nyadhifa zao hadi pale uhusika
wao katika sakata la NYS utakapo bainishwa.
Katika
taarifa yake kwa waandishi wa Habari, Raila alisema watatu hao, lazima wajiuzulu
kupisha uchunguzi kama walivyofanya baadhi ya Mawaziri waliotuhumiwa katika
sakata mbalimbali walivyofanya mwaka 2015.
“Baadhi ya
mawaziri walilazimika kujiuzulu baada ya kutuhumiwa katika sakata mbalimbali za
kujihusisha na ufisadi. Sheria iliyotumika dhidi Charity Ngilu, Kazungu Kambi,
Felix Koskei, Davis Chirchir na Michael Kamau lazima itumike dhidi ya
watuhumiwa wote wa kashfa ya NYS,” ilieleza taarifa hiyo.
Kiongozi huyo
wa kambi rasmi ya upinzani, alienda mbali kwa kudai kwamba wakenya, wamepoteza
matumaini na imani kwa viongozi wao, na kuongeza kwamba Duale, Murkomen na
Rotich lazima wawajibike hadi watakapothibitika kutohusika.
“Viongozi hawa wamezima matumaini na imani ya
Wakenya, wanapaswa kuwajibishwa kwa hilo, kitu cha muhimu cha kufanya kwa sasa
ni kujiuzulu na kupisha uchunguzi,” ilifafanua.
Duale na
Murkomen ambao ni kutoka kambi ya Naibu Rais, Willium Ruto, wamepinga vikali
madai ya Waiguru, na kusema kuwa hakuna ukweli wowote nyuma ya kiapo chake,
kauli ambayo ilimsukuma Raila kuamini kuwa wawili hawa wanatumia viabaya
madaraka yao.
“Ukiwa unalipwa ili uwawakilishe wakenya
katika baraza la bunge la taifa na lile la Senate, uwapiganie matakwa yao na
uwatatulie matatizo yao, huwezi kutumia dhamana hiyo kuwaibia, huwezi kutumia
wadhifa wako kuwachukulia wanaokushtumu kuwasaliti wakenya kuwa ni wapuuzi,”
ilisema taarifa ya Raila.
Wakati
huo huo, Kiongozi wa Taifa wa chama cha Amani National Congress (ANC), Musalia
Mudavadi, amemtaka Rais Uhuru Kenyatta kuhakikisha anaongoza vita dhidi ya
Ufisadi.
Akizungumza
katika ibada ya mazishi, kijijini Kamimei, kaunti ya nandi, Mudavadi alisema
kuwa, kasi ya ufisadi nchini inatisha. Aliwasihi viongozi waliotajwa kuhusika
na ufisadi kuwajibika bila kucheza mchezo wa kutuhumiana.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :