SOMALIA: AL SHABAAB YAUA MASHABIKI 24 WA SOKA WAKIANGALIA MECHI YA MAN UTD VS ARSENAL
Posted in
afrika mashariki
No comments
Sunday, February 28, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
![]() |
Ukumbi wa Mkahawa ulioshambuliwa na Al Shabaab |
MASHABIKI wa Soka wapatao 24 wameuawa mjini Baidoa
Kusini mwa Somalia wakitizama mechi baina ya Manchester United na
Arsenal baada ya shambulizi lililotekelezwa na Al Shabab.
Miongoni mwa wale waliouawa ni pamoja na afisa wa serikali ya jiji hilo. Mji wa Baidoa ulitekwa na wapiganaji waislamu wa Al-Shabaab mwaka wa 2008, lakini walitimuliwa mwaka 2012.
Mji huo ulioko takriban kilomita 200 kutoka mji mkuu Mogadishu ni mji wa hivi punde zaidi kushambuliwa na wanamgambo hao wa kiislamu.
Shambulizi la kwanza lilitokea katika mgahawa maarufu unaopendwa na wageni na viongozi wa kisiasa ambao ulishambuliwa kwa gari lililokuwa limetegwa bomu. Walionusurika waliokolewa na wanajeshi wa muungano wa Afrika AMISOM.
Shambulizi hili limetokea muda mchache tu baada ya kukamilika kwa warsha ya viongozi wa mataifa yanayochangia wanajeshi wake katika jeshi la muungano wa Afrika AMISOM. Siku ya ijumaa watu wengine zaidi ya 20 waliuawa katika mgahawa mwengine kufuatia shambulizi la Al Shabaab.
Chanzo: BBC SWAHILI
Habari Zingine
- WENGI WALIVYOJITOKEZA KUMUAGA MWANA TBN JENNIFER LIVIGHA (CHINGA ONE) HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR
- Wachimbaji mgodi 15 waliokwama ardhini waokolewa nchini Tanzania
- Al-Shabab washambulia kambi ya majeshi ya Kenya nchini Somalia
- UHURU WA HABARI SIO KUIANGALIA TU SERIKALI - MWAKYEMBE
- JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA LATANGAZA KUSUSIA KUANDIKA HABARI ZA MKUU WA MKOA WA DAR
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :