ARUSHA: SOUTH SUDAN YAJIUNGA RASMI AFRIKA MASHARIKI

No comments
Wednesday, March 2, 2016 By danielmjema.blogspot.com

JUMUIYA ya Afrika Mashariki, imekubali ombi la uanachama lililowasilishwa na taifa la Sudan Kusini na hivyo kufanya nchi wanachama wa jumuiya hiyo kufikia sita ikiwa na jumla ya watu wapatao milioni 162.

Uamuzi huo ulifikia leo, katika mkutano wa 17 wa wakuu wa nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki -EAC-, unaoendelea mjini Arusha nchini Tanzania, chini ya Uenyakiti wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

“Sudan kusini, ni mwanachama mpya wa EAC,” ilisema taarifa rasmi ya sekretariet ya EACuliochapishwa leo katika ukurasa wa mtandao wake.

Taarifa kutoka makao makuu ya EAC, mjini Arusha ilitangaza kuwa swala la Sudan Kusini ilikuwa ni moja ya Ajenda za mkutano huo. ilisema kuwa viongozi wangeamua katika mjadala dhidi ya ombi la Sudan Kusini la kujuinga na jumuiya hiyo kati ya maswala mengine yaliyopangwa kujadiliwa.

Sudan Kusini ambayo iliwasilisha ombi la kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mara ya kwanza mara baaada ya kujitenga kutoka taifa la Sudan, mnamo mwaka 2011, sasa inajiunga na Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda and Burundi.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .