KENYA: WAFUASI WA JUBILEE NA KANU WAGOMBEA ENEO LA KAMPENI, UCHAGUZI MDOGO WA SENATE, KAUNTI YA KERICHO
Posted in
afrika mashariki
No comments
Saturday, March 5, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
WAFUASI wa vyama vinavyokinzana vikali kwenye uchaguzi mdogo wa kiti cha Senate katika Kaunti ya Kericho, chama cha Kenya National Union (KANU) na chama tawala cha Jubilee vimejikuta vikigombea eneo la kufanyia kampeni, asubuhi ya leo, kitendo kilicholazimisha Jeshi la polisi kutumia Bomu ya kutoa machozi kutuliza ghasia zilizoanza kuibuka.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na kituo cha Television cha Citizen, Polisi walilazimika kuchukua hatua hiyo baada ya umati mkubwa wa wafuasi wa pande zote mbili kuonesha hali ya kutaka kuzichapa, kila upande kikidai uhalali wa kuendesha kampeni zake katika eneo la Uhuru Gardens, mjini Kericho.
Kundi la KANU, lililokuwa likiongozwa na Nick Salat na Alfred Keter, lilikuwa likisisitiza kuwa, wao ndio wenye kibali halali cha kutumia eneo hilo kwa shughuli zao za kampeni kutokana na kile walichodai kuwa, walikuwa wa kwanza kuomba eneo hilo kabla ya Jubilee.
Taarifa zaidi zinadai kuwa, Mkuu wa Jeshi la polisi katika kaunti ya Kericho (OCPD) akiwa pamoja na kikosi cha kutuliza ghasia, alifika katika eneo hilo na kuwazuia wafuasi wa KANU, kuweka mahema yao tayari kwa kufaya kampeni.
KANU ambayo inaonekana kuwa ni mpinzani mkubwa wa Chama tawala cha Jubilee katika uchaguzi huo utakaofanyika, siku ya Jumatatu, inadaiwa kulipia Kericho green stadium kwa ajili ya shughuli ya kufunga kampeni, itakayoendeshwa na mgombea wake, Paul Sang.
The curtains come down on the Kericho Senate contest
Saturday with the Jubilee party and KANU combing various villages in
search of votes for their respective candidates.
KANU and Jubilee, siku ya jana, walifanya mikutano zaidi ya 10 kila mmoja katika harakati za kuwashawishi wapiga kura kuwachagua wagombea wao. uchaguzi huo mdogo utakaofanyika siku ya Jumatatu, unaonekana kama mzani wa kupima nguvu ya Makamu ya Rais, William Ruto katika ukanda wa Bonde la ufa (Rift Valley region).
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :