TANZANIA: RAIS DKT. MAGUFULI AMEMTEUA BALOZI KIJAZI KUCHUKUA NAFASI YA BALOZI SEFUE
Habari zilizotufikia hivi punde, zinasema kuwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua, Balozi Mhandisi John William Kijazi (pichani) kuwa Katibu mkuu Kiongozi wa nchi hiyo.
Kwa mujibu taarifa Rasmi, kwa vyombo vya Habari, iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu ya Tanzania, Gerson Msigwa, zinadai kwamba Balozi Kijazi ambaye kabla ya uteuzi wake, alikuwa ni Balozi wa Tanzania nchini India anachukua nafasi ya Balozi Ombeni Sefue.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa kufuatia uteuzi huo, Balozi Sefue ambaye amehudumu tangia Awamu ya Nne chini ya Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, sasa atapangiwa kazi nyingine.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :