NAIROBI: RAIA WA KENYA WANAOTUMIKIA KIFUNGO 'UGHAIBUNI' KURUDISHWA NYUMBANI

No comments
Friday, March 11, 2016 By danielmjema.blogspot.com

WAKENYA wanaotumikia kifungo katika magereza nje ya mipaka ya nchi, sasa watarudishwa nyumbani endapo mazungumzo kuhusu uwezekano wa uhamisho wa wafungwa baina ya nchi husika itazaa matunda.

Mapendekezo hayo yaliyochini ya kanuni za kubadilishana wafungwa, pia yanatarajiwa kujumuisha masharti ya kufanya uhamisho ikiwa ni pamoja na uwepesi wa kuhamisha wafungwa ndani na nje ya mipaka ya Kenya.

Jaji mkuu wa Kenya, Willy Mutunga amethibitisha kuwa mswada huo utaunda msingi wa mpango wa kubadilishana wafungwa kati ya Serikali ya Kenya na nchi wabia wa mpango huo. inadaiwa kuwa karibia wafungwa  3,000 wenye uraia wa Kenya wanatumikia vifungo katika nchi mbalimbali kote duniani huku Kenya nayo ikiwa na idadi kubwa tu ya wafungwa wa kigeni.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .