LUCY KIBAKI ALAZWA ICU

No comments
Friday, March 11, 2016 By danielmjema.blogspot.com

MKE wa Rais wa Awamu ya tatu wa Kenya, Mwai Kibaki, mama Lucy Kibaki, amelazwa katika chumba cha wagonjwa wenye hitaji la uangalizi mkubwa (ICU), akiwa katika hali mbaya, baada ya kukimbizwa Hospitalini, siku ya jana (Alhamisi), kutokana na kuugua ghafla akiwa nyumbani kwake, Muthaiga, jijini Nairobi.


Mama Lucy, alikimbizwa katika Hospitali ya Gertrude Children’s Hospital, kwa ajili ya huduma ya dharura kuokoa maisha kabla ya kuhamishiwa Nairobi Hospital.

“Ni kweli kuwa mke wa Rais zamani wa Kenya, yuko hapa Hospitalini kwetu, tumelazimika kumpeleka ICU,” chanzo chetu katika Hospitali ya Nairobi kiliiambia Gazeti la The Star na kuongeza kuwa Mama Lucy ambaye amekuwa kimya tangu mwaka 2010, anasumbuliwa na tatizo la kupumua (breathing difficulties)".

Mwaka 2014, Mama Lucy alikimbizwa Hospitalini baada ya kulalamika kuwa anasikia maumivu kifuani na mara ya mwisho kuonekana hadharani ni katika sherehe ya uzinduzi wa Katiba mpya, iliyofanyika katika uwanja wa Uhuru Park.


Chanzo: The Star


Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .