TANZANIA: MSOMI KUTOKA TANZANIA KUWANIA TUZO YA SAYANSI
Posted in
afrika mashariki
No comments
Friday, March 11, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Msomi mmoja kutoka Tanzania Aneth
David Mwakilili ni miongoni mwa wasomi wengine walioteuliwa kuwania tuzo
la wanasayansi wachanga barani afrika maarufu kama The Next Einstein
Forum (NEF).
Aneth ni mwanafunzi wa MSc, mwaka wa mwisho, katika chuo kikuu cha Dar es salaam ambaye utafiti wake wa sasa, imejikita katika kuchunguza ubora wa bacteria kwa kiingereza 'effectiveness of Bacillus strains
as biocontrol, biofertilizer and biopreservative agents, and genomic
comparison of the strains'.
Msomi huyu, anapenda kujikita katika uchugunzi wa maswala ya kilimo (agricultural
biotechnology, agricultural bioinformatics and policies affecting
translation of scientific discoveries into viable solutions).
Tuzo hiyo huleta pamoja wasomi wa sayansi, watunga
sheria na washika dau katika seKta mbali mbali barani afrika, kujadili
na kuhimiza sayansi inayoweza kutatua matatizo yanayokumba bara la
Afrika.
Washindi wa tuzo hiyo wanapewa ufadhili na usaidizi kutoka kwa wakfu huo ili kutekeleza utafiti wao kikamilifu. Katika shindano hili Mwakilili, atafanya utafiti ambao utasaidia wakulimu kutokomeza kwekwe na hivyo kuimarisha mazao yao.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :