SAA ZENYE UWEZO WA KUIBIA MITIHANI ZABUNIWA!
Posted in
Teknolojia
No comments
Friday, March 4, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
KUA UYAONE! nchini Kenya utasikia neno la "Mwakenya" kwenye vyumba vya kufanyia mitihani. hizi ni karatasi yaliyoandikwa majibu kwa lengo la kuiba mitihani, wakati mwingine pia wanafunzi huandika majibu kwenye mapaja au sehemu yoyote mwilini.
Yote hayo ni kwa lengo moja tu; kuiba mitihani, sasa nakupa kitu kipya!! Watalamu ya sayansi wamebuni Saa za kisasa ambazo zimetengenezwa mahususi kutumiwa kudanganya wakati wa mtihani zimekuwa zikiwakosesha usingizi walimu na wasimamizi wa mitihani. Saa hizo zina uwezo wa kuweka akiba data na maelezo ambayo yanaweza kusomeka mtu anapofanya mtihani.
Aidha, zina kitufe cha dharura ambacho kinaweza kubadili uso wa saa hizo haraka sana na badala ya kuonesha habari ziwe zinaonesha uso wa kawaida wa saa. Saa hizo zinatangazwa katika soko la kuuza bidhaa mtandaoni la Amazon.
Mojawapo ya aina ya saa hizo ina uwezo wa kuweka akiba data ya 4GB. Nyingine, ambayo itaanza kuuzwa baadaye mwaka huu, itakuwa na uwezo wa 8GB na inaweza kuhifadhi hata video. Baadhi ya saa hizo, zina kifaa kidogo sana cha kusikizia ambacho hakitumii nyaya, jambo linalowezesha mtu kusikiliza kilichohifadhiwa kwenye saa hiyo bila kuonekana.
- Udanganyifu wa mitihani ni kawaida India
- Visa vya wizi mtihani wa taifa Kenya vyaongezeka
- Watafutaji kazi walazimishwa kuvua nguo India
Kuna pia matangazo ya saa hizo eBay.
Naibu mwalimu mkuu wa shule moja kutoka Bath, Uingereza anasema saa hizo zinaweza zikawashawishi wanafunzi kuhadaa katika mtihani.
Bw Joe Sidders wa shule ya Monkton Combe Senior School amesema ingawa saa hizo zinaweza kudhibitiwa kwa kutumia sheria zinazoharamisha simu na kompyuta kutoka vyumba vya mitihani, ni changamoto kubwa sana kwa watu wanaosimamia mitihani.
Amesema uuzaji wa saa hizo unafaa kudhibitiwa.
Kuna pia “kalamu za kuiba mtihani” ambazo zinaweza kuhifadhi habari na maelezo.
Ongezeko la matumizi ya saa kuiba yamefanya baadhi ya mashirika kupiga marufuku saa katika vyumba vya mitihani Uingereza.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :