SOMALIA: TEMBO ARUDI NYUMBANI BAADA YA MIAKA 20
Posted in
afrika mashariki
No comments
Thursday, March 10, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Ndovu mmoja kwa jina Morgan
amefanikiwa kuvuka mpaka na kuingia nchini Somalia mwezi huu, na kuwa
mara ya kwanza ndovu huyo kuonekana nchini humo tangu miaka 20
iliyopita.
Safari yake imewashangaza watunza mazingira ambao wanasema kuwa hatua hiyo inaonyesha kuwa ndovu huyo alikumbuka njia za zamani baada ya miongo kadha ya kuondoka Somalia kutokana na mapigano.
Safari ya Morgan ni ishara tosha kuwa eneo la mpaka kati ya Kenya na Somalia, linaonekana kuboreka kiusalama na ikiwa hali itakuwa shwari kusini mwa Somalia, basi ndovu waishio uhamishoni watarudi nyumbani.
Kutoka ene la Tana River Morgan alitembea umbali wa kilomita ishirini usiku wa kwanza kabla ya kujificha ndani ya msitu mkubwa na kuendelea na safari siku iliyofuata . Alirudia mtindo huo kwa siku 18.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :