KENYA: MCHORA KATUNI 'GADO' KUMSHITAKI BOSI WAKE
Posted in
afrika mashariki
No comments
Thursday, March 10, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Mchoraji vibonzo wa Kenya Godfrey
Mwapembwa ,aka Gado ameiambia BBC kwamba atalishtaki gazeti la The daily
Nation nchini Kenya kuhusu kile alichokitaja kuwa kusimamishwa kwa
kandarasi yake kinyume cha sheria.
Mhariri wake katika gazeti hilo alipendekeza kwamba apumzike kwa kuwa sio mfanyikazi kamili wa gazeti hilo lakini amepewa kandarasi ya kuchora vibonzo hadi mwezi Julai 2016. Hatahivyo mwezi uliopita alipewa barua ya kumsimamisha kazi.
Gazeti hilo limesisitiza kuwa uamuzi huo wa kuachana uliafikiwa na pande zote mbili,lakini mchoraji huyo anaamini kwamba kufutwa kwake kulitokana na shinikizo za kisiasa akiongezea kuwa anaamini kwamba serikali ya Uhuru Kenyatta imekuwa haipendezwi na kazi.
Mwapembwa ni mchora vibonzo maarufu nchini Kenya ambaye huwachekesha wasomaji wengi kwa uchoroji wake. Mtandao wake unaomtaja kuwa mchoraji vibonzo hodari wa kisiasa katika eneo la mashariki na Afrika ya kati,anasema kuwa vibonzo vyake huangazia kila swala kutoka ugaidi,ukataji miti,ukimwi na ufisadi na vibonzo vyake vimekuwa vikizua mjadala mkubwa.
SOURCE: BBC SWAHILI
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :