UGANDA: OFISI ZA MAWAKILI WA MBAMBAZI ZAVAMIWA
Posted in
afrika mashariki
No comments
Wednesday, March 9, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Ofisi mbili za mawakili wanaomuakilisha aliyekuwa waziri mkuu wa Uganda, Amama Mbabazi katika kesi yake kupinga ushindi wa rais Yoweri Museveni katika uchaguzi uliomalizika zimevamiwa na watu wasiojulikana jana usiku.
Mohamed Mbabazi, wakili anayeongoza mawakili wengine katika kesi hiyo ya Mbabazi, amesema vipakatilishi, tarakilishi na nyaraka zilichukuliwa kutoka ofisi yake.
Afisa mmoja wa ulinzi alipigwa na watu walioivamia ofisi hiyo. Ofisi nyengine iliyoingiliwa ni ya wakili Fred Muwema. Polisi Uganda wanasema wanafanya uchunguzi.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :