UJERUMANI: KASISI MWEUSI AJIUZULU AKIHOFIA MAISHA YAKE
Posted in
Kimataifa
No comments
Monday, March 7, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Kasisi mkatoliki mzaliwa wa Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kati DRC amelazimika kujiuzulu kazi yake nchini
Ujerumani baada ya kutishiwa maisha.
''Kwa kweli tumepigwa na butwa kufuatia vitisho hivyo dhidi ya maisha ya kasisi Ndjimbi-Tshiende'' taarifa iliyochapishwa katika tovuti ya kanisa hilo inasema. Uhasama umeibuka kati ya kasisi Ndjimbi-Tshiende na wanasiasa wa jimbo hilo wanaoshikilia msimamo mkali wa chama cha CSU.
Yamkini kasisi huyo Ndjimbi-Tshiende alitofautiana na kiongozi wa chama hicho cha CSU Sylvia Boher mwezi Oktoba kufuatia matamshi yake. Boher alikuwa amezungumzia kuhusu uvamizi wa wahamiaji kutoka Eritrea waliokuwa wametoroka kutumikia jeshi la taifa lao.
Baada ya maoni hayo ya kasisi Ndjimbi-Tshiende, mwanasiasa wa chama cha CSU rafiki ya Boher, bwana Johann Haindl, alimtusi kasisi huyo hadharani.
Viongozi hao wawili walituhumiwa na umma na wakalazimika kujiuzulu nyadhfa zao chamani. Chama cha Christian Social Union (CSU) kinamuunga mkono kansela wa Ujerumani Angela Merkel na chama chake cha Christian Democrats (CDU).
Polisi sasa wanaendelea na uchunguzi wa ubaguzi wa rangi na tishio dhidi ya kasisi Ndjimbi-Tshiende. Ujerumani inakabilia na upinzani mkali dhidi ya hatua ya kansela wa Ujerumani kuwapokea wakimbizi milioni 1.1. Vyombo vya habari vinaripoti kuwa kasisi huyo ametishiwa maisha mara tano.
Chanzo: BBC Swahili
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :