UTURUKI: MLIPUKO MKUBWA WAUA WATU 27

No comments
Monday, March 14, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Kumetokea mlipuko mkubwa katikati ya mji mkuu wa Uturuki, Ankara. Afisa muandamizi wa usalama, anasema kuwa takriban watu 27 wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa. 
Maafisa wa usalama wanakisia idadi ya wale waliojeruhiwa kuwa ni 75.

Mlipuko huo uliwasha moto magari yaliyokuwa yameegeshwa karibu na kituo kikubwa cha mabasi na bustani katika mtaa wa Kizilay. Vyombo vya habari vya Uturuki vinasema mlipuko ulitokana na bomu lilotegwa kwenye gari.

Mwezi uliopita, Ankara ilishambuliwa kwa bomu lilouwa karibu watu 30. Maafisa wakuu wa Uturuki wakati huo, waliwalaumu wapiganaji wa Kikurd.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .