IVORY COAST: WAVAMIZI WAUA WATU 12 HOTELINI
Posted in
Habari na Jicho Pevu la Kijiwe
No comments
Monday, March 14, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Watu 12 wamepigwa risasi na kuuawa 4
kati yao watalii katika shambulizi lililoteka muda mfupi uliopita
katika hoteli moja ya kifahari nchini Ivory Coast. Msemaji wa polisi anasema kuwa 4 hao ni raia wa Ulaya walikuwa nchini humo kwa likizo.
Picha za Video zinaonesha miili ya watu ikiwa imetapakaa sakafuni kwenye ufunkwe wa Grand Bassam, karibu na mji mkuu wa Abidjan. Walioshuhudia wanasema kuwa wavamizi hao waliokuwa wamejihami kwa bunduki za rashasha walivamia mgahawa wa kifahari wa L'Etoile du Sud.
Hoteli hiyo ya kitalii ya Grand Bassam Ivory Coast, iko takriban kilomita 40 kutoka mji mkuu wa Abidjan. Walioshuhudia uvamizi huo wanasema kuwa wavamivi waliokuwa wamejihami kwa bunduki za rashasha waliwafyatulia risasi watalii waliokuwa wakijivinjari kwenye ufukwe huo maarufu sana na watalii.
Wavamizi hao walikuwa wamejifunika uso. Hata hivyo video ambazo hazijathibitishwa zimechapishwa kwenye mitandao ikiwaonesha watalii wakikimbia kuokoa maisha yao huku mtu aliye na bunduki akifyatua risasi.
Ivory Coast imekuwa kisiwa cha amani magharibi mwa Afrika hadi pale tofauti za kisiasa zilipoibuka mwaka wa 2002 kati ya wenyeji wa Kaskazini na wale wa Kusini. Tangu hapo nchi hiyo imekuwa ikishuhudia hali ya amani ambayo kila mara inatibuliwa na mapigano.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :