JE, UMEWAHI KUWAZA MAISHA BILA MITANDAO YA KIJAMII?
Posted in
Teknolojia
No comments
Monday, March 14, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Facebook, Snapchat, Instagram, Twitter, Whatsapp - mitandao ya kijamii
ambayo yamegubika maisha ya watu katika muongo uliopita lakini matumizi
yake yametanda kwa ukubwa kiasi cha kuwa kwa baadhi imekuwa ni kama
uraibu.
Sasa wanafunzi elfu moja wa Cheshire wanajaribu kubaini maisha yalikuwaje enzi za kabla ya uvumbuzi wa mitandao hiyo ya kijamii. Shirika la Habari la BBC, imewapa changamoto wanafunzi wa shule ya upili ya Tarporley kukaa bila ya kutumia mitandao hiyo kwa wiki moja.
Baadhi
ya watu wazima huenda wanaona ni jambo rahisi, kwasababu sio kuwa simu
za wanafunzi hao zinachukuliwa, na bado wanaruhusiwa kupiga simu kutuma
barua pepe au hata ujumbe mfupi. Lakini mtihani huu mpaka sasa umedhihirisha jinsi vijana wanavyotegemea sana mitandao hiyo ya kijamii katika maisha yao.
Wanafunzi watatu wanaarifu jinsi mtihani huu ulivyokuwa kwao : "Fikra
ya kuwasiliana moja kwa moja au pengine kusoma kitabu mara nyengine
inaonekana kuwa jambo gumu. Ni wengi wanaokiri kucheza michezo katika
mitandao lakini kila mtu inaonekana anatumia mitandao ya kijamii kila
siku."
Mwalimu mmoja amesema anakaribisha mtihani huo: "mitandao
ya kijamii imegubika mno maisha ya watu binafsi, kiasi cha kugeuka kuwa
uraibu." Lakini iwapo umepokonywa njia yako kuu ya kuwasiliana huedna hilo ni tatizo.
Daisy,
mwenye umri wa miaka 14, anasema aliupokea mtihani huo vizuri,
aligundua kwamba wiki iliopita alitumia saa 16 katika snapchat na
ametazamia wiki isiyokuwa na shinikizo la kutaka kuitazama simu yake saa
zote.
Lakini mwishoni mwa juma amegundua kuwa hilo sio
rahisi:"Ilibidi nizime ujumbe usiingie kwenye simu ili nisishikwe na
hamu ya kuitazama simu yangu." Amegundua mbinu za zamani za mawasiliano kama kutuma barua pepe kwa marafiki walio ng'ambo na pia kupiga simu.
"Sio
kuwa ni uraibu, ninaendelea na maisha ya kawaida," anasema Georgia
mwenye umri wa miaka 15 kuhusu anavyotumia mitandao ya kijamii. Lakini awali alikuwa na waiwasi kuhusu namna rafiki zake wangellimikiria kwa kuotea tu ghafla kutoka mitandao hiyo.
Kuona
ujumbe wa snapchat katika simu yake na kuupuza imekuwa vigumu kwake,
lakini: "nimekuwa nikitazama magazeti na majarida," anasema, "na
kuzungumzana wazazi wangu kuhusu mambo mengine kando na wao kuwa
madereva wangu wa taxi!"
Kati ya wanafunzi hao 1,000 walioanza tihani huo wa kukaa bila ya kutumia mitandao ya kijamii, karibu robo wamekiri kushindwa. Miongoni mwao ni Sam, alipohitajika kuwasiliana na rafiki yake kucheza tenisi na akagundua hana nambari yake ya simu kumpigia.
Hana nambari ya simu ya mtu yoyote kwenye simu yake, kwa hiyo suluhu ilikuwa ni kutumia snapchat.
Inavyoonekana
ni kama wanafunzi wengi watafurahia wakati mtihani huo utakapokamilika
ili waweze kurudi katika enzi ya kisasa ya mawasiliano.
Lakini
maktaba ya shule ya upili ya Tarporley huenda ingependa mtihani huo
uendelee - msimamizi wake anasema hajawahi kushudia idadi kubwa ya
vitabu kuombwa kama ilivyokuwa katika wiki iliopita.
Chanzo: BBC Swahili
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :