KENYA YAENDELEA KUIKALIA ICC KOONI, SASA YATAKA KUKABIDHIWA FAILI ZA WASHUKIWA 3
Posted in
afrika mashariki
No comments
Thursday, April 21, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Kenya sasa inataka faili za kesi
zinazowakabili wakenya watatu wanaotuhumiwa kuingilia ushahidi wa
mashahidi wa ICC kushtakiwa nchini humo. Mwanasheria mkuu Profesa
Githu Muigai amesema kuwa Kenya ina mahakama zilizo na uwezo za kushtaki
kesi ndogo kufuatia kuanguka kwa kesi kuu iliowahusisha wakenya sita
maarufu kama Ocampo 6.
Mwanasheria huyo pia ameshtumu idara ya mashtaka katika mahakama ya ICC kwa kushindwa kushirikiana na Kenya kuhusu ombi la awali lililowasilishwa kwa aliyekuwa kiongozi wa mashtaka Moreno Ocampo kuikabidhi Kenya faili zote za washukiwa.
Amesema kuwa Kenya ina haki ya kushirikiana na mahakama hiyo au la iwapo ICC itafeli kuikabidhi Kenya faili hizo. Ameongezea kuwa mpango wa Kenya kujiondoa katika mahakama hiyo utaangaziwa na Umoja wa Afrika AU na kwamba Kenya kama taifa haijaanza harakati za kujiondoa.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :