MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA (TCRA) KUWABANA WASANII WANAOPOSTI PICHA ZA UTUPU
Posted in
afrika mashariki
No comments
Thursday, April 14, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Akizungumza na mtandao huu mwishoni mwa wiki iliyopita, Meneja
Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, Innocent Mungi alisema ingawa jukumu la
kuwakamata wote wanaoweka picha zinazokiuka maadili ni la jeshi la
polisi kupitia kitengo cha makosa ya mtandao (Cyber Crime), taasisi hiyo
inawasiliana na wamiliki wa mitandao ya kijamii ili kutafuta namna
nzuri ya kuwadhibiti.
“Tunachofanya ni kuzungumza na hawa watu ili kuwafungia wote
wanaokiuka maadili, tunajua baadhi yao wanajiunga katika mitandao kwa
kutumia majina ya uongo, lakini sisi tutazifungia ‘line’ maana kila moja
ina namba zake za siri na hazifanani na zingine, hivyo ukiondolewa kwa
kufungiwa huwezi tena kujiunga kwa vile kule kwenye mitandao wanatambua
namba,” alisema.Katika mitandao hiyo, baadhi ya wasichana wakiwemo maarufu, wamekuwa wakiweka picha zinazokiuka maadili, kwa sababu mbalimbali wengine wakitajwa kuwa wanajiuza.
Baadhi wa wasichana wenye majina maarufu ambao wamekuwa wakitupia picha zenye utata mara kwa mara katika mitandao licha ya Lulu ni pamoja na Agnes Gerald ‘Masogange’, Gigy Money, Shilole, Kidoa, Anti Lulu, Isabela Mpanda na wengineo.
Chanzo:GPL
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :