RASMI: ANTHONIO CONTE NDIO MRITHI WA MOURINHO CHELSEA

Posted in
No comments
Monday, April 4, 2016 By danielmjema.blogspot.com

KLABU ya Chelsea, inayoshiriki ligi kuu ya Barclays, English Premier League, Imemthibitisha rasmi Kocha, Antonio Conte kuwa meneja wa klabu hiyo, akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Jose Mourinho.


Mourinho alitimuliwa klabuni hapo mwanzoni mwa msimu huu, kufuatia matokeo mabaya na nafasi ya umeneja ikashikiliwa kwa muda na Mdachi, Guus Hiddink ambaye amefanya kazi kubwa kuinusuru klabu hiyo yenye maskani yake Kaskazini mwa London na aibu ya kushuka daraja ambapo mpaka sasa zikiwa zimesalia takribani mechi 7, ligi itamatike, The Blues inashikilia nafasi ya 10.

Conte ambaye ni kocha wa zamani wa Juventus, kwa sasa anakinoa kikosi cha timu ya taifa ya, 'The Azzuri', lakini mwezi mmoja uliopita alikaririwa akidai kuwa atajiuzulu wadhifa wake kama kocha mkuu wa Azzuri baada ya kumalizika kwa michuano ya ubingwa wa Ulaya, Euro 2016, itakayofanyika nchini Ufaransa.

Mkataba

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 46, amekuwa akihusisha na mpango wa kuhamia Chelsea kwa muda mrefu sasa, ambapo leo, Machi 4, 2016, uongozi wa Mabingwa hao watetezi wa EPL wameamua kuvunja ukimya na kumtangaza Conte ambaye atachukua jukumu la kuinoa Chelsea baada ya Euro.

Taarifa zilizochapishwa katika mtandao rasmi wa www.chelseafc.com, zinasema kwamba Uongozi wa klabu hiyo na Conte wamefikiwa mwafaka wa kuingia mkataba wa miaka mitatu.

"Nimefarijika sana kupata fursa ya kuwa Meneja wa Chelsea, ninafuraha kuwa kocha wa timu ya taifa ya taifa langu na sasa kazi na jukumu la kifahari kama la kuwa Meneja wa Chelsea linakuja mbele yangu, nategemea kukutana na kila mtu klabuni hapo, na zaidi ni kuwa tayari kwa mapambano kwenye EPL," alisema Conte.
 
Mataji aliyotwaa

Enzi za uchezaji wake, Conte alifanikiwa kutwaa mataji 15 katika klabu ya Juventus kabla ya kuja kuiongoza kutwaa taji la Serie A, mara tatu mtawalia (2011/2012, 2012/2013, 2013/2014) ikawa nii rekodi nyingine kwani mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa ni miaka ya 1930.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .