RIEK MACHAR AZUA HOFU, JE ATAREJEA JUBA, YUKO WAPI?
Posted in
afrika mashariki
No comments
Wednesday, April 20, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lina wasiwasi mkubwa kuhusiana na
kushindwa kwa Riek Machar kurejea mjini Juba kwa ajili ya kuchukua
wadhifa wa makamu wa rais na kufungua njia ya kuundwa serikali mpy.
Hata hivyo hadi kufikia wakati huu Machar hajawasili mjini mkuu juba na badala yake msemaji wake William Ezekiel ameeleza.
''Tunataka kuwaarifu kwamba Dr Riek Machar makamu wa kwanza wa rais mtarajiwa ambaye anatakiwa kuwasili hatowasili leo mpaka itakapotangazwa tena sababu bila shaka inahusiana na mipangilio ya usafiri. Ndege iliyotakiwa kumbeba mkuu wa majeshi ya SPLA katika chama cha SPLM upinzani jenerali Simon Garwich haijapewa idhini ya kutumia anga ya Sudan Kusini''
Ni kauli hii na kutowasili kwa Machar ndiko kulikoutia wasiwasi Umoja wa Mataifa.Mkuu anayehusika na masuala ya amani katika Umoja huo Herve Ladsous ameliarifu juu ya hali ya Sudan Kusini baraza la usalama la Umoja huo lenye wanachama 15 kufuatia ombi la Marekani,kwamba hali iliyopo nchini humo inatia wasiwasi.
China ambayo kwa mwezi huu wa Aprili ndiyo inayoshikilia uwenyekiti wa baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa,kupitia naibu balozi wake katika Umoja huo Wu Haitao imesema wanachama wa baraza hilo wamesisitiza utayarifu wao wa kushughulikia hatua yoyote itakayojitokeza ya kutatiza utekelezaji wa makubaliano ya amani ya Sudan Kusini.
Kwa mujibu wa balozi wa Urusi ndani ya Umoja huo, Peter Llichev alichokibaini Ladsous ni kwamba kuna hali ya kutoaminiana kwa kiasi kikubwa kati ya pande hizo mbili ingawa mjumbe huyo wa amani ameelezea pia matumaini kwamba Machar huenda akawasili Jumatano mjini Juba.
Maelfu ya wasudan Kusini waliuwawa na zaidi ya milioni 2 katika nchi ya watu milioni 11 wameachwa bila makaazi kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili ya mapigano yaliyozuka mwishoni mwa mwaka 2013, ikiwa ni chini ya miaka miwili baada ya taifa hilo kujipatia uhuru wake. Mzozo huo ulitokana na kutimuliwa kwa Machar serikalini na rais Kiir na kuzua vita ambavyo viligeuka kuwa vya kikabila kati ya Dinka kabila la rais Kiir dhidi ya Nuer kabila la Machar.
Mwandishi: Saumu Mwasimba
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :