WAFANYAKAZI HEWA WAMPONZA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA, NCHINI TANZANIA
Posted in
afrika mashariki
No comments
Monday, April 11, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga kutokana na kuwepo kwa watumishi hewa. Bi Anna Kilango Malecela alitangaza kwenye vyombo vya habari kuwa mkoa wake hakuwa na watumishi hewa.
Ikulu hata hivyo ilifanya uchunguzi wake na kubaini kuwepo kwa wafanyakazi hewa 45 katika awamu ya kwanza. Awamu ya pili ya uchunguzi huo bado inaendelea katika wilaya mbili za Ushetu na Shinyanga Vijijini.
Akiongea Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema amesikitishwa na hali hiyo na kuagiza mkuu huyo wa mkoa na Katibu Tawala wa Mkoa Abdul Rashid Dachi kuondolewa kazini mara moja.
"Na wale wote wa Shinyanga ambao walisemekana ni zero, hakuna mtumishi hewa, walikuwa tayari wameshalipwa shilingi milioni 339.9, nimejiuliza sana, na nikajiuliza sana na kwa kweli nimejiuliza sana na kwa masikitiko makubwa, kwa nini mkuu wa mkoa alisema hakuna mtumishi hewa?" amesema Dkt Magufuli.
Kwa jumla, zaidi ya wafanyakazi hewa 2,000 waligunduliwa baada ya utathmini kufanywa mikoani.
Habari Zingine
- JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA LATANGAZA KUSUSIA KUANDIKA HABARI ZA MKUU WA MKOA WA DAR
- WENGI WALIVYOJITOKEZA KUMUAGA MWANA TBN JENNIFER LIVIGHA (CHINGA ONE) HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR
- Wachimbaji mgodi 15 waliokwama ardhini waokolewa nchini Tanzania
- Al-Shabab washambulia kambi ya majeshi ya Kenya nchini Somalia
- UHURU WA HABARI SIO KUIANGALIA TU SERIKALI - MWAKYEMBE
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :