Bondia Manny Pacquiao amechaguliwa kuwa Seneta wa Bunge la Ufilipino

Posted in
No comments
Thursday, May 19, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Bondia mwenye jina kubwa katika ulimwengu wa ngumi Manny  May 19 2016 ameingia kwenye headlines baada ya kufanikiwa kushinda nafasi ya Seneta katika bunge nyumbani kwao FilipinoPacquiao amefanikiwa kushinda nafasi hiyo kwa kura milioni 16.
Pacquiao anakuwa ni miongoni mwa watu 12 waliofanikiwa kushinda nafasi ya Seneta katika bunge la Filipino, ushindi wa bondia huyo maarufu unatoa tafsiri huenda siku akapata nafasi ya kugombea nafasi za juu za uongozi wa nchi hiyo hususani Rais.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Manny Pacquiao mwenye umri wa miaka 37 amefanikiwa kushinda mataji kadhaa ya Ubingwa ngumi, Pacquiao ndio bondia aliyepigana na Mayweather na kupoteza kwa point katika pambano linalotajwa kutazamwa na mamilioni ya watu duniani kote.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .