China yatengeneza mabasi yanayopita juu ya magari mengine (tizama Video)

Posted in
No comments
Wednesday, May 25, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Umewahi kusikia ule msemo unaosema, 'Dunia isimame nipande?' hii sasa ni zaidi ya hiyo, China imekuja na uvumbuzi mpya ambapo, hivi karibuni wametengeneza Mabasi ya mwendo kasi, yanayotumia umeme, yanayopita juu ya magari mengine barabarani! 
Usishangae, kwani kadri Teknolojia inavyozidi kukua kila siku katika upande wa usafirishaji ndivyo ufumbuzi wa baadhi ya changamoto zinavyozidi kupatiwa majibu, kama ilivyo kwa Tanzania ilivyoleta mabasi yaendayo haraka ili kuepuka foleni, ndivyo hivyo imetokea Beijing China ambapo wao wameweza kutengeneza basi la umeme lenye uwezo wa kupita juu ya magari mengine.
Kutokana na China kuwa nchi yenye watu wengi zaidi Duniani, hivyo basi hilo linalotajwa kubeba watu 1200 kwa mara moja, linatajwa kuwa ufumbuzi sahihi wa msongamano wa magari barabarani, basi hilo lilifanyiwa majaribio kwa mara ya kwanza May 19 2016.
Cheki Video ya Mabasi hayo yakiwa safarini:

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .