Diamond ndani tuzo za BET awards 2016
Posted in
afrika mashariki
,
Burudani
No comments
Friday, May 20, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Kazi imeanza tena, yule mkali wa kuwanyoosha kwenye tuzo mbali mbali, ametueliwa tena kuwania tuzo ya BET awards 2016. Msanii wa Bongo fleva anayendelea kukimbiza na kuitangaza muziki wa Afrika Mashariki, Diamond Platnumz kutoka Tanzania ametueliwa kuwania tuzo hiyo pamoja na mastaa wengine wakubwa akiwemo Rihanna na Beyonce.
Diamond amekuwa msanii pekee kutoka Afrika Mashariki kutajwa kuwani tuzo hiyo ambapo ameingia katika kipengele cha Msanii Bora wa Kimataifa toka Africa.
Diamond ameshukuru kwa kuchaguliwa kuwania tuzo kwenye kipengele cha Best international Act Africa ambapo ameyaandika maneno haya baada ya kufikiwa na taarifa "Ningependa niwashukuru kwa Sapoti kubwa Manayozidi kunipa na niwajuze kuwa kijana wenu nimechaguli kuwania tunzo ya Msanii Bora wa Kimataifa toka Africa kwenye tunzo za BET #BETAwards America"
Tuzo za BET 2016 ambazo zitatolewa nchini Marekani zimeanza kuchukua nafasi kwenye headlines baada ya kutangazwa list ya waliochaguliwa kuwania tuzo hiyo huku Beyonce, Rihanna na Drake wakitangazwa kuongoza kwa kuwania tuzo zaidi ya moja.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :