Vita ya Jaydee na Gardner imefikia patamu
Baada ya siku saba kupita tangu Msanii Judith Wambura 'Lady Jaydee' kumfikishia barua ya Mwanasheria akimtaka aliyekuwa mume wake, Gardner G. Habash kumwomba radhi hadharani, mtangazaji huyo amejibu mapigo.
Mtangazaji huyo amedai kuwa kauli aliyoitoa hivi karibuni, haikuwa inamzungumzia mwanamuziki huyo huyo kama ilivyotafsiriwa. Kauli hii imefuata baada ya siku 21 kupita tangu Gardner, ambaye ni mtangazaji wa Clouds FM, kudaiwa kutoa lugha ya udhalilishaji inayodaiwa kumlenga mwenza wake huyo wa zamani.
Gardner anadaiwa kutamka maneno hayo ya udhalilishaji Mei 6, mwaka huu na kurekodiwa kisha video kusambazwa katika mitandao ya kijamii, katika ukumbi wa CDS park alipokuwa akisherehesha Tamasha la Miss TIA 2016.
Hata hivyo, kupitia Mwanasheria wake Stephen Axweso kutoka kampuni ya Brevis Attorney, Gardner amekana tuhuma zinazomkabili za kumdhalilisha aliyekuwa mkewe. "Mteja wetu hajafanya kosa lolote lisilo la kisheria dhii ya mlalamikaji na kwamba kwa kipndi chote alichokuwa akisherehesha hakuna jina la mteja wako, hivyo haikuwa na maana kwamba aliyekuwa binti wa kike ni mteja wako," ilisema barua hiyo.
Mwanasheria huyo alisema mteja wake ana maono mabaya dhidi ya uhusiano wake wa zamani, "Kwa hili ninakuomba usome kwa mara nyingine kuhus sheria za masuala ya talaka ili uweze kumwongoza vizuri mteja wako, tafadhali naomba utambue kwamba mteja wetu ameyakataa madai ya mteja wako."
Barua hiyo iliyoandikwa na Wakili Stephen Axweso iliambatanishwa kwa kampuni tano ikiwemo Clouds Media East Africa, Rockstar 4000, President Tanzania Institute of Accountancy Students Organization (TASO), Hartman Traders na Bronx Entertainment.
Mwanasheria wa Jaydee
Mei 13, mwaka huu, kupitia Mwanasheria wake, Amani Tenga kutoka kampuni ya Law Associates Advocate, Lady Jaydee, alimwandikia barua ya kumtaka mtangazaji wa Clouds FM, Gardner Habash kuomba radhi mbele ya umma ndani ya siku saba kwa kauli ya udhalilishaji aliyoitoa dhidi yake.
Taarifa iliyosomeka katika barua hiyo ya Mwanasheria ilimtaka Gardner aombe radhi ba iwapo akikaidi, atachukuliwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kesi ya udhalilishaji na kashfa.
Gardner alipoulizwa na Gazeti la Mwanaspoti, toleo la Kenya, alijibu: "Sina maoni yoyote kuhusu jambo hili." Barua iliyoandikwa na Mwanasheria huyo ilisomeka kuwa kauli ya Gardner, maneno yake hayo yalikuwa yakimhusu Jaydee moja kwa moja hivyo kusababisha udhalilishaji mbele ya umma.
"Kutokana na udhalilishaji huo, mteja wetu ameathirika kwa namna nyingi, moja ikiwa ni kumletea sifa mbaya kama mwanamke mbele ya umma, kuhatarisha shughuli zake za kibiashara za kila siku ambazo ni muziki na burudani." Kilieleza kipengele cha tatu cha barua hiyo.
Kipengele cha nne kilieleza; "Mteja wetu ameumia kisaikolojia na baadhi ya masilahi yake yameathirika kwa kiasi kikubwa sana, ukizingatia maneno hayo yameendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari.
Kibano
Mwanasheria huyo alisema iwapo wawili hao walishapeana talaka chini ya Sheria za Ndoa za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inakataza mtu kuongelea jambo lolote linalohusu mambo ya ndoa.
Aidha, barua hiyo ilimkanya Gardner kuhakikisha anakamilisha utaratibu aliopewa kwa wakati na iwapo atashindwa kutekeleza agizo hilo, itamlazimu kulipia gharama za usumbufu katika hatua za kisheria zitakazochukuliwa.
Ilielezwa kuwa wadhamini na waandaji wote wa Tamasha la Miss TIA 2016, wanaweza kuchukuliwa hatua za kisheria pia kutokana na tamasha hilo kutumika kumkejeli na kumdhalilisha mwanamuziki huyo.
Siku moja baada ya mtangazaji huyo kutoa kauli hiyo hadharani, Naibu waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Dk Hamis Kigwangalla alisema kitendo hicho cha udhalilishaji, si tu kwa mwanamuziki huyo bali ametukana wanawake wote.
"Nikiwa Balozi wa Wanawake natoa rai kwa uongozi wa Clouds FM kumtaka Gardner afute kauli yakena aombe radhi kwa Jaydee na umma ili kulinda heshima yao," aliandika Kigwagalla kupitia ukurasa wake wa twitter.
Mwandishi: Herieth Makwetta
Chanzo: Mwanaspoti Kenya
Habari Zingine
- JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA LATANGAZA KUSUSIA KUANDIKA HABARI ZA MKUU WA MKOA WA DAR
- WENGI WALIVYOJITOKEZA KUMUAGA MWANA TBN JENNIFER LIVIGHA (CHINGA ONE) HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR
- Wachimbaji mgodi 15 waliokwama ardhini waokolewa nchini Tanzania
- Al-Shabab washambulia kambi ya majeshi ya Kenya nchini Somalia
- RAPPER WA CAMEROON, NGOMA AACHIA VIDEO YA WIMBO MPYA ‘ALL LES DAY’, AIELEZEA COLLABO YAKE NA RAY VANNY
- New Hit: Lady Jay Dee – Sawa Na Wao
- Madonna atembelea makazi duni ya Kibera, Nairobi
- Timbulo: SIjarejea kwenye ualimu
- Vijana wazidi kujitokeza usaili wa Maisha Plus East Africa, Dar es salaam yatia fora
- UHURU WA HABARI SIO KUIANGALIA TU SERIKALI - MWAKYEMBE
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :