FIFA yamtangaza Katibu Mkuu wa kwanza Mwanamke

Posted in
No comments
Saturday, May 14, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA leo May 13 2016 limetangaza kwa mara ya kwanza katibu mkuu mwanamke katika historia ya shirikisho hilo, FIFA imemtangaza Fatma Samba Diouf Samoura kutoka Senegal kuwa katibu mkuu wa kwanza wa shirikisho la hilo mwanamke.
Rais wa sasa wa FIFA Gianni Infantino, wakati akimtangaza Samoura kuwa katibu mkuu wa shirikisho hilo.

Fatma Samba Diouf Samoura anaingia FIFA mwezi June kuanza kazi rasmi na kurithi nafasi ya Jerome Valcke katibu mkuu wa shirikisho hilo aliyefungiwa miaka 12 kutokujihusisha na soka, Samoura mwenye miaka 54 ametangazwa leo katika mkutano uliofanyika Mexico.

ukumbi wa mkutano wa 66 wa FIFA
FIFA imemtangaza Fatma Samba Diouf Samoura ambaye CV yake inaonesha kuwa amewahi kufanya kazi katika umoja wa mataifa UN kwa miaka 21, mabadiliko hayo yamefanyika ikiwa ni muendelezo wa mabadiliko katika shirikisho hilo, baada ya Rais wa zamani wa shirikisho hilo Sepp Blatter kuachia ngazi.
Fatma Samba Diouf Samoura

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .