Kenya yaendelea na msako dhidi ya ISIS
Posted in
afrika mashariki
No comments
Thursday, May 26, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Polisi nchini Kenya inaendelea na msako wa kuutia mbaroni mtandao wa kundi la wapiganaji la ISIS ambalo linataka kukita mizizi yake nchini Kenya kwa lengo la kufanya mashambulizi ya kigaidi dhidi ya wananchi wasio kuwa na hatia.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na inspekta mkuu wa polisi. Kauli hiyo imetolewa baada ya polisi nchini Kenya kuwatia mbaroni watu wawili wanaoshukiwa kuwa ni wafuasi wa kundi la wapiganaji la ISIS.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na inspekta mkuu wa polisi. Kauli hiyo imetolewa baada ya polisi nchini Kenya kuwatia mbaroni watu wawili wanaoshukiwa kuwa ni wafuasi wa kundi la wapiganaji la ISIS.
Kwa mujibu wa polisi, kukamatwa kwa wawili hao ambao ni Mwangolo Mgutu na Abubakar Jillo Mohammed kumezuia mashambulizi ya kigaidi yaliyokuwa yakipangwa kwa kutumia vilipuzi na silaha nyingine katika mji wa Nairobi na Mombasa.
Mbali na kukamatwa kwa washukiwa hao wawili, polisi pia imepata vitu mbalimbali katika nyumba ya Kiguzo Mwangolo kama vile misumari, betri, waya na mbolea ambazo inadaiwa zingetumika kutungezea bomu la nyumbani.
Polisi imeendelea kusema, katika uchunguzi wake wa mwanzo, imebaini kuwa Kiguzo na Abubakar ni miongoni mwa waandishi wa makala iliyokuwa inasambaa kupitia mtandao ambao ilikuwa ikielezea kuwepo kwa kundi la Jahba katika eneo la Afrika Mashariki ambalo limetangaza kumuunga mkono kiongozi wa ISIS Abubakr Al-Baghdadi.
BBC
BBC
Habari Zingine
- UHURU WA HABARI SIO KUIANGALIA TU SERIKALI - MWAKYEMBE
- JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA LATANGAZA KUSUSIA KUANDIKA HABARI ZA MKUU WA MKOA WA DAR
- WENGI WALIVYOJITOKEZA KUMUAGA MWANA TBN JENNIFER LIVIGHA (CHINGA ONE) HOSPITALI YA AMANA JIJINI DAR
- Wachimbaji mgodi 15 waliokwama ardhini waokolewa nchini Tanzania
- Al-Shabab washambulia kambi ya majeshi ya Kenya nchini Somalia
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :