Msikilize Kumwembe anavyochambua uamuzi uliochukuliwa na Man United kumtimua Van Gaal

Posted in
No comments
Thursday, May 26, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Bado wapenzi na mashabiki wa Man United wanasubiri ile siku atakayotangazwa rasmi kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Louis van Gaal ndani ya klabu ya Man United. kupitia Ayo TV, Mchambuzi mahiri wa soka, Afrika mashariki na kati, Edo Kumwembe, anakuletea tathmini yake .
“Ni kweli Van Gaal alikuwa anahitaji muda zaidi wa kujenga timu, kwani Van Gaal ana CV kubwa katika vilabu alivyopita ila anahitaji misimu mitatu minne ili aweze kupata mafanikio, halafu Van Gaal sio kocha wa kufundisha mastaa huwa anawapa nafasi wachezaji wachanga”
“Kwa Man United kwa sasa wanahitaji kujenga image ya klabu yao ambayo itaiwezesha kulinda brand yao ya biashara, hivyo Mourinho ni mtu sahihi kuitoa shimoni klabu hiyo, kwani Mourinho ni kocha mwenye rekodi ya kutwaa mataji katika msimu wake wa kwanza” mtizame Kumwembe anavyoshusha tathmini:

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .