Nyasi kuwaka moto leo Uwanja wa Nyayo, Gor Mahia Vs Mathare

Posted in
No comments
Sunday, May 22, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Klabu ya Mathare United iliyo katika nafasi ya pili kwenye Jedwali la msimamo watakuwa na kibarua kigumu cha kuikabili Gor Mahia iliyo katika nafasi ya nne, pointi (tatu nyuma ya Ulinzi), kwenye mchezo wa raundi ya 14,Ligi kuu ya KPL, utakaopigwa kwenye dimba la Nyayo, mjini Nairobi kuanzia majira ya saa 10:00 aliasiri. 
Mechi hii itakuwa ni kipimo cha muelekeo wa Kogalo ambao ni mabingwa watetezi wa taji la ligi, huku ikiwa moja ya mechi ngumu inayotazamiwa na wengi kutumika kutathmini uwezo wa Kocha Mbrazili, Jose Marcello 'Ze Maria' huku kwa Kocha Francis Kimanzi huu ukiwa ni mtihani mkubwa kwake kuhakikisha anawaondoa wasiwasi mashabiki wa Mathare na kuwahikikisha kuwa Mathare imerejea rasmi katika utawala wa soka la Kenya.
Wakati Kogalo watakuwa wanahitaji kupanda katika nafasi ya pili (kutokana na tofauti ya mabao), Mathare watakuwa na kila sababu ya kupambana kushinda mechi hii kwani itawapa uhakika wa kukalia usukani, kwa pointi 29, pointi moja zaidi ya Tusker FC iliyolazimishwa sare 1-1 na SoNy Sugar jana.
Ushindi katika mchezo wa leo, utatoa taswira ya Kogalo inayoendelea kufukuzia taji la la nne kimya kimya chini ya uongozi wa Kocha mwenye roho ya Paka, Ze Maria ambaye ameiwezesha Gor Mahia kuepuka aibu ya kushindwa kutamba na kuonesha makali yao ya msimu uliopita.
Endapo Kogalo watafanikiwa kuifunga Mathare, watapanda hadi nafasi ya pili kutokana na tofauti ya idadi ya mabao ya kufunga ambapo Gor Mahia wana mabao 8 zaidi ya Mathare.
Akizungumzia mechi ya Leo, Kimanzi alisema kwake anaamini lolote linaweza kutokea na tayari ameshaanda vijana wake kwa ajili ya mtanange huo kwani anafahamu ugumu wa Kogalo hasa katika michezo mikubwa kama hii.
“Nimekuwa nikisema mara kwa mara, mimi kwangu kila mechi ni kama fainali, sijawahi kubeza uwezo wa wapinzani wangu, nafahamu Gor Mahia ni timu ngumu hivyo nimejiandaa kuwakabili, mechi hii ni muhimu sana kwetu," alisema Kimanzi
Jacques Tuyisenge of Gor Mahia FC tackles Nelson Marasoweo of Ushururu FC during their KPL Top 8 Knockout tournament match at the Nyayo National stadium on May 02, 2016.[Photo/SPORTPICHA]
Jacques Tuyisenge wa Gor Mahia, akikabiliana na Nelson Marasoweo wa Ushuru katika mechi ya hivi karibuni.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .