Sauti Sol kupeleka Tour ya 'Live and Die in Africa, Mozambique na South Africa.

Posted in
No comments
Tuesday, May 24, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Kundi la muziki la Sauti Sol wanaotamba katika muziki wa Afro Poo wakiwa na vibao vikali kama vile Unconditionally Bae, sasa wameamua kuhamishia 'Tour' ya 'Live and Die in Africa' nchini Msumbuji (Mozambique) na Afrika kusini (South Africa)
Wakiwa katika Ziara ya kutangaza albamu yao hiyo (Live and Die in Africa) kundi hilo limefanikiwa kuzunguka katika nchi nyingi ndani na nje ya bara la Afrika ambapo sasa wameamua kupiga kambi nchini Msumbji na Bondeni kwa Mandela kwa lengo la kuwafikia mashabiki wao walioko huko.
Sauti Sol wanatumia ziara hiyo kutambulisha nyimbo zao 15 zilizoko kwenye albamu hiyo ikiwa ni pamoja na kupiga nyimbo zao nyingine ambapo hivi majuzi tu walikamilisha ziara kwa mikoa ya Kenya.
Kwa mujibu wa ratiba yao, Kundi hili lililojizolea sifa duniani kutokana na aina ya uimbaji wao, wanatarajiwa kufanya onesho katika tamasha la Azgo Festival, nchini Mozambique, Mei 21, mwaka huu na kisha kuelekea Carfax, Jijini Johanesburg, South Africa, Mei 27, kabla ya kurejea nchini Mozambique ambapo watatumbuiza kwenye Bushfire Festival, mjini Maputo,Mei 28.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .