Nuh Mziwanda: Shilole amenilostisha Kinoma

Posted in
No comments
Tuesday, May 24, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Nuh Mziwanda amedai katika miaka mitatu aliyokuwa na uhusiano na Shilole amepoteza mambo mengi. Akiongea na mtandao wa burudani nchini Tanzania, Bongo5, Nuh amesema hakuna zaidi anachokumbuka kwenye uhusiano huo zaidi ya majuto.


“Kuna vitu muhimu sana ambavyo nimegundua ningeweza kuvifanya na ningekuwa nipo mbali sana,” amesema Nuh. Muimbaji huyo amesema uhusiano huo ulimfanya auchukulie poa muziki na hivyo kushindwa kutengeneza hit song.
Anasema Shilole alihakikisha katika muda wote waliokuwa nao Nuh asihit kwa uoga kuwa akiwa staa atamuacha.
“Yule [Shilole] alikuwa na trick nyingi za kunifanya mimi nijionee staa tayari, nijione mimi napendwa na watu au mimi muziki wangu unavuma kumbe bado halafu yeye huku muziki wake unaenda,” amesisitiza.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .