TID: Hakuna kama Ngwea
Posted in
Burudani
No comments
Saturday, May 28, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Msanii mkongwe wa Bongo fleva, TID anasema mpaka sasa kwenye maisha yake ya muziki hajaona msanii ambaye ataweza kuchukua nafasi ya aliyekuwa mkali wa ‘free style’ bongo, Albert Mangwea, aliyefariki miaka mitatu iliyopita.
TID akijibu swali aliloulizwa na mtangazaji wa kipindi cha Friday Night Live cha EATV, Sam Misago, aliyemuuliza iwapo kuna msanii yeyote anayefikia uwezo wa Ngwea.
‘What are u saying…! Ngwea!? Hakuna msanii anayeweza kumfikia Ngwea, that man was special, Ngwea alikuwa blessed! Halafu umfananishe na nani…Bill Nas anaweza kuwa a half of it lakini hawezi kuwa kama Ngwea, Ngwea can rap, Ngwea can sing, Ngwea can give u a melody..halafu umfananishe na mtu, hakuna wa kufanana naye, no one!”, alisikika TID akijibu. Leo ni miaka mitatu tangu kifo cha rapper huyo aliyefariki nchini Afrika Kusini.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :