UN yaishauri Kenya kutokufunga Kambi ya wakimbizi

No comments
Tuesday, May 10, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia wakimbizi UNHCR limeitaka serikali ya Kenya kubatilisha msimamo wake wa kutaka kuzifunga kambi mbili za wakimbizi za Dadaab na Kakuma nchini humo.

Serikali ilisema Ijumaa iliopita kwamba kambi hizo mbili zitafungwa kufuatia wasiwasi wa usalama na ukosefu wa fedha. Ilitoa tangazo kama hilo awali,lakini wakati huu serikali imesema kuwa inazifunga idare zake za wakimbizi katika kile kinachoonekana kama hatua ya kwanza ya kusitisha uhifadhi wa wakimbizi 600,000.
Wengi wao ni raia wa Somalia na Sudan Kusini.'Tumelipokea na wasiwasi mkubwa tangazo hilo'',lilisema shirika hilo katika taarifa yake.Iliongezea:
La kushangaza ni kwamba hali ilivyo Somalia na Sudan Kusini inayowafanya raia kutoroka haijatatuliwa.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .