Diamond: Nikisema nisainiwe na lebo nyingine, ntakuwa nabana riziki za wengine

Posted in
No comments
Saturday, June 4, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Hivi karibuni bosi wa WCB, Diamond Platnumz alitoa kauli iliyowatoa povu baadhi ya mashabiki wa muziki kwa kuitafsiri kauli hiyo kuwa anamuonea gere msanii mwenzake, Alikiba baada ya kusaini dili mpya na record label ya Sony Music.

Akiongea kwenye kipindi cha Clouds E, kinachoruka kupitia Clouds TV, Diamond alisema, “Mungu kanisaidia nikadunduliza kupata kidogo changu hicho hicho ambacho nimekiinvest ambacho nafanyia shughuli yangu. Mimi nikasainiwe record label nyingine ni uongo ni kama naenda kubana riziki za watu wengine. Nimeshafanya nyimbo karibia na wasanii wote wa Afrika sasa hivi nina macollabo na wasanii wa Marekani.”
“Nikiwa labda nina uwezo wa kusema nimpigie fulani na fulani nikapate hiyo hela nikafanya kwanini nikasaini record label? Ni sawa sawa na kwenda kulitoa pato la Tanzania kuwapelekea watu bure ilhali tunaweza tukafanya wenyewe tukapata riziki, ni heri nikae nyumbani,” aliongeza.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .