Gigy Money: Nay wa Mitego anaimba Taarab, sio Hip Hop

Posted in
No comments
Friday, June 3, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Video Queen asiyeisha vituko, Gigy Money amerushia dongo Nay wa Mitego na kudai kwamba Staa huyo anaimba Hip Hop kama Taarab hivyo kumtaka kubadilika.


Gigy ambaye hapo awali amewahi kuzinguana na hitmaker huyo wa ‘Nasaka Pesa’ baada ya kutumika kwenye video ya Shika Adabu Yako ya rapper huyo na kutolipwa ujira wake, amemuambia mtangazaji wa Jembe FM ya Mwanza, JJ kuwa hip hop ya Nay imejaa uswahili mwingi.
“Inabidi abadilishe uimbaji wake uwe wa kisasa zaidi. Nay anaimba hip hop as taarab, imekuwa ni lugha ya mafumbo wakati hip hop ni zamani ilikuwa inatritiwa nyimbo sexy ambazo anasikiliza mtu akiwa ametulia,maneno unayasikia,” amesema Gigy. “Lakini yeye anataka kuimba vitu vingi katika muda mmoja halafu anaponda, so he is bad to me kwa asilimia 00.0.”
Kwa upande mwingine Gigy amesema msanii wa hip hop anayemkubali Tanzania ni Joh Makini. “Anajielewa, hana skendo, yaani ana nyota yake kali, msafi,” amesisitiza. “Anaimba vizuri, unamsikia hata kama ni M-Arusha, yaani R na L zinatofautiana.”

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .