Jaji aamuru kesi ya Besigye ifanyikie Mahakamani na sio Gerezani

No comments
Wednesday, June 15, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Kizza Besigye

Kesi ya Uhaini dhidi ya kiongozi wa Upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, ambaye alikuwa ni mpinzani mkuu wa Rais Yoweri Museveni, sasa kusikiliziwa Mahakamani. 

Hilo ni kwa mujibu wa Amri Jaji mmoja nchini humo ambaye ameagiza kesi dhidi ya kiongozi huyo ambaye Chama chake cha Forum for Democratic Change (FDC) kilipoteza katika uchaguzi mkuu uliopita, ifanyike mahakamani kwa makosa ya uhaini na wala sio kwenye gereza lenye ulinzi mkali ambapo anazuiliwa.
Besigye alifikishwa mahakamani kwa muda mfupi ambapo kesi yake iliahairisha hadi tarehe 29 mwezi Juni. Mwendesha mashtaka aliomba kesi hiyo kufanyika mahakamani kutokana na sababu za kiusalama.
Alikamatwa mwezi uliopita na kushtakiwa kwa uhaini baada ya kupanga sherehe za kuapishwa kwake kama rais. Alipinga ushindi wa Rais Yoweri Museveni wa awamu ya tano wa uchaguzi wa mwezi Februari.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .