Rais Kenyatta amewasili Brussels, Ubelgiji, kwa ajili ya mkutano mkubwa wa EU kuhusu Maendeleo
Posted in
afrika mashariki
No comments
Wednesday, June 15, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Rais Uhuru Kenyatta (picha kutoka Maktaba) |
Rais Uhuru Kenyatta amewasili mjini Brussels, Ubelgiji mapema leo, ambapo anatarajiwa kuhudhuria Kongamano la Siku za maendeleo za mataifa ya Ulaya, lijulikanalo kama, European Development Days (EDD).
Katika ziara hiyo ya siku tatu, Rais Kenyatta anatatarajiwa kuhutubia kongamano hilo pamoja na kushiriki mazungumzo kadhaa kuhusu Usalama na Biashara.
Katika Hotuba yake, Rais Kenyatta anatarajiwa kuwashirikisha wajumbe wa baraza la umoja la Ulaya, kuhusu uzoefu wa Kenya katika maswala mbalimbali pamoja na kuanisha mitazamo kadhaa ya taifa la Kenya kuhusu mshikamano ya kibiashara na utangamano katika siku zijazo.
Rais Kenyatta pia atafanya mazungumzo kadhaa na baadhi ya maafisa wakuu wa Umoja wa Ulaya, akiwemo Rais wa EU, Jean Claude Juncker na Rais wa Kamati kuu ya Ulaya, Donal Tusk.
Aidha, Rais Kenyatta pia atafanya kikao cha ndani na Waziri Mkuu Michel pamoja na Mfalme Philipe wa Ubelgiji. Rais atafanya mazungumzo ya ujirani mwema na Serikali ya Ubelgiji, atahutubia Jumuiya ya Biashara ya Ubelgiji na hatimaye kuhudhuria mkutano kati ya EU na Afrika.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Rais Kenyatta pia anatazamiwa kukutuna na Wakurugenzi wakuu wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya, European Investment Bank (EIB), ambapo pia atakutana na maafisa wengine wakuu wa sekta ya Biashara.
Jumuiya ya Ulaya ni mshirika namba mbili wa Kenya katika maswala Maendeleo, Biashara na mmoja wa vyanzo vizuri vya Uwekezaji, Foreign Direct Investment (FDI) na mshirika mkuu wa Utalii.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :