Kha! eti Panya 200 kutumika katika maandamano nchini Kenya

No comments
Wednesday, June 15, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Ukistaajabu ya Musa, Utaona ya Firauni!. Huko nchini Kenya katika mji wa Nyeri mkoa wa kati, waandamanaji wanapanga kuwatumia panya 200 katika maandamano yao, gazeti la the Star la nchini humo limeripoti.

Gazeti hilo limemnukuu mshirikishi wa maandamano hayo John Wamagata akisema “tutaleta panya 200 na kuwatembeza katikati ya mji”.

Gazeti hilo linaongezea kwamba maandamano hayo yanayopangwa kufanyika wiki ijayo yanapinga mapendekezo ya bunge la kaunti hiyo kutumia shilingi milioni 75 kujenga klabu ya kuimarisha afya.
Klabu hiyo itakuwa na eneo la kunyosha misuli, eneo la kuoga kwa kutumia mvuke,eneo la masaji,kidimbwi cha kuogelea na sauna kulingana na gazeti la the star.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .