Payet na Griezman waipeleka Ufaransa 16 bora, Euro 2016
Posted in
Michezo
No comments
Thursday, June 16, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Magoli mawili ya dakika za lala salama kutoka kwa Antoine Griezmann na Dimitri Payet dhidi ya Albania, yanaipeleka Ufaransa hadi hatua ya mtoano ya michuano ya Euro 2016.
Albania waligongesha mwamba muda mchache baada ya kipindi cha pili kuanza wakati Ledian Memushaj unganisha krosi iliyompita golikipa wa Ufaransa Hugo Lloris.
Straika wa Ufaransa na Arsenal Olivier Giroud pia shuti lake liligonga mwamba kabla ya Griezmann aliyetokea benchi kuiadhibu safu ya ulinzi ya Albania kwa kuunganisha kwa kichwa krosi ya Adil Rami.
Payet akakandamiza bao la pili na kuihakikishia Ufaransa ushindi unaoipa tiketi ya kufuzu kucheza hatua ya 16 bora ya mashindano hayo.
Kichapo hicho ni kichungu kwa Albania ambao walionekana kufanya kazi ya ziada ili kupata ushindi wa kwanza kwenye michuano ya Ulaya kwenye uwanja wa Stade Velodrome huko Marseille.
Ufaransa walisubiri goli la dakika za lala salama la Payet ili kupata ushindi kwenye mchezo wa ufunguzi uliochezwa Ijumaa dhidi ya Romania, ushindi wa leo umewahakikishia kucheza hatua ya mtoano kabla ya mchezo wao wa mwisho wa Kundi A dhidi ya Switzerland.
Albania ambao walipoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Switzerland, lazima waifunge Romania kwenye mechi yao ya Jumapili licha ya kwamba hawana tena nafasi ya kufuzu kusonga mbele.
- Kingsley Coman (miaka 20 na siku mbili) ni mchezaji mdogo zaidi kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Ufaransa kwenye fainali za michuno mikubwa, amevunja rekodi ya Bruno Bellone aliyecheza michuano ya kombe la dunia mwaka 1982 (alikuwa na miaka 20 na siku 118)
- Mchezo huu wa michuano ya Ulaya ulikuwa ni wa kwanza kushuhudiwa ukienda mapumziko bila timu yeyote kupiga shuti lililolenga goli tangu mwaka 2008 kwenye mchezo Euro kati ya Ufaransa dhidi ya Romania.
- Goli la Griezmann lilikuwa la kwanza kutoka kwa mchezaji aliyeingia akitokea benchi kwenye michuano ya Ulaya tangu fainali za mwaka 2000 dhidi ya Italy (Sylvain Wiltord na David Trezeguet).
- Magoli matatu ya Ufaransa kati ya manne kwenye michuano hii inayoendelea yamefungwa kuanzia dakika ya 89 na kuendelea.
- Payet mpaka ameshachangia magoli matatu ya Ufaransa (magoli mawili amefunga na assist moja) jambo linalomuweka sawa na Zinadine zidane ambaye alifanya hivyo mwaka 2004.
- Albania wameruhusu goli la mapema na goli la dakika za mwisho zaidi hadi sasa, goli lao la mapema lilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Switzerland (dakika 5 baada ya mchezo kuanza) wakati la dakika za mwishoni lilikiwa ni dhidi ya Ufaransa, goli lililofungwa na Payet dakika ya 90+6
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :