Niki wa Pili awachana Wasanii wanaishi maisha ya kuiga

Posted in
No comments
Friday, June 3, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Msanii msomi wa Hip Hop Bongo, Niki wa Pili amewachana baadhi ya wasanii wanaoishi maisha ya kuigiza yasiyokuwa na uhalisia. Ni kweli wasanii wengi bongo wanaongoza kwa kuishi maisha ya kuigiza tofauti na kipato wanachokipata.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Nick wa Pili alisema, “Sisi watu maarufu wasanii waigizaji ni watu ambao tunaonekana ni kioo cha jamii, ni role model, ni mfano wa kuigwa, lakini mimi nimejaribu kuangalia hivi kweli sisi ni watu role model? Na jamii kama wanatuiga sisi wanaiga vitu sahihi?.”
“Kwa mfano sisi wasanii maisha yetu wengi ni feki tunavyoonyesha kwenye instagram, tunayosema kwenye media sio vitu vya kweli, alafu vijana wanatuiga, itakuwa mapokeo gani kwenye jamii? Saa kama vijana wanaiga vitu feki kutakuwa na matokeo gani kwenye jamii?,” aliongeza. Wimbo wake Role Model uliotoka Alhamis unazungumzia mambo hayo pia.


Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .