MKURUGENZI WA JAMII FORUMS AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA MARA YA PILI

No comments
Monday, December 19, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Mwanzilishi wa mtandao maarufu nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla wa Jamii Forums, Maxence Melo anatarajia kufikihwa Mahakamani Asubuhi ya leo, katika Mahakama ya Kisutu, Jijini Dar es salaam.

Maxence Melo, ambaye ni Mkurugenzi wa Jamii Media.Co Ltd, alikamatwa juma lililopita akikabiliwa na mashitaka matatu ambayo yalitajwa mbele ya Mahakimu watatu, mnamo Desemba 16, mwaka huu kuwa ni:

1. Kumiliki tovuti ambayo haijasajiliwa Tanzania.
2. Kuzuia uchunguzi wa Jeshi la Polisi.
3. kushindwa kutoa data alizonazo kuhusu watumiaji wa mtandao huo.

Licha ya kufikishwa Mahakamani, Matumanini ya Melo kupata dhamana baada ya kusota mahabusu ya Polisi kwa siku tatu tangu akamatwe, yaligonga mwamba kwa kukosa wadhamini wenye vigezo katika shtaka la tatu na hivyo kulazimika kurudishwa rumande hadi leo ambapo atapandishwa tena kizimbani.

Ilikuwa kama sinema kwa kuwa awali Melo baada ya kupandishwa kwa Hakimu Victoria Nongwa alipata dhamana na kuachiwa huru, lakini Polisi walimkamata tena na kumrudisha kwa Hakimu Godfrey Mwambapa ambako nako dhamana ilikuwa wazi, ila alishindwa kutimiza masharti na kupelekwa rumande.

Kesi tatu alizofunguliwa katika kikao hicho cha kwanza cha Desemba 16 ni kumiliki tovuti ambayo haijasajiliwa nchini Tanzania, na mbili za kuzuia uchunguzi wa wa Jeshi la Polisi kinyume na sheria ya makosa ya kimtandao (Cybercrime Act).

Awali katika kesi namba 458/2016 mbele ya Hakimu Nongwa, Wakili wa Serikali, Mohammed Salum alidai kuwa kati ya Desemba 9, 2011 na Deseba 13, 2016, katika eneo la Mikocheni, Wilaya ya Kinondoni, Jijini Dar es salaam, Melo akiwa Mkurugenzi wa Jamii Media inayoendesha tovuti ya Jamii Forums, aliutumia mtandao huo ambao haujasajiliwa katika anuani za tovuti nchini humo (.co.tz)

Pia alidaiwa kuwa, akiwa anajua kuwa Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi kuhusiana na mawasiliano ya kimtandao ambayo yalichapishwa katika tovuti yake, alizuia uchunguzi huo kwa kushindwa kutekeleza amri ya kutoa Data alizokuwa nazo.

Baada ya kukamilisha masharti ya dhamana, aliachiwa huru lakini muda mfupi baadaye akakamatwa tena na kufikishwa mbele ya Hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba na kusomewa shtaka lingine katika kesi namba 456/2016. 

Leo ni matarajio ya wengi hasa wanahabari wenzake kwamba, Melo atafanikiwa kukamilisha mashrti ya dhamana na kuachiwa huru. tutaendelea kuwajuza kuhusu yanayojiri Mahakamani...ungana nasi katika mtandao wetu wa Instagram @kutoka254 upate Updates kuhusu kesi hii

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .