TAARIFA YA TANZANIA BLOGGERS NETWORK (TBN) KWA WAANDISHI WA HABARI TAREHE 02 DESEMBA, 2016 KATIKA UKUMBI WA IDARA YA HABARI (MAELEZO)
Posted in
afrika mashariki
No comments
Friday, December 2, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Ndugu Mwakilishi kutoka Benki ya NMB,
Waandishi wa habari,
Kwa
niaba ya Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii nchini 'Tanzania
Bloggers Network' (TBN) napenda kuwashukuru kwa kujitokeza katika mkutano huu
muhimu. TBN inajua kuwa mnamajukumu mengi ya kuujuza umma masuala anuai, lakini
mmechagua kuja kwetu ili kutusikiliza tulichowaitia na baadae tunaamini mtaujuza
umma juu ya tukio letu.
TBN
iliosajiliwa rasmi na Serikali mwezi Aprili, 2015 kwa kushirikiana na wataalam
wa masuala ya habari na mitandao ya kijamii imeandaa semina kwa wanahabari hawa
wa mitandao ya kijamii hasa 'Bloggers' itakayofanyika jijini Dar es Salaam.
Semina hii maalumu ambayo itajumuisha mafunzo ya siku mbili yaani tarehe 5 na 6
ya Mwezi Desemba, 2016 kwa washiriki takribani 150 kutoka Tanzania nzima (Bara
na Visiwani) itafuatiwa na mkutano mkuu kwa wanachama hai wa TBN kujadili
masuala mbalimbali ya chama na tasnia nzima ya mitandao ya jamii.
Ndugu Wanahabari,
Katika
mkusanyiko huu wanatasnia watapewa semina juu ya uendeshaji mitandao ya jamii
kwa manufaa, upashaji habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuziangatia maadili
na namna ya kunufaika na mitandao hiyo kwa waendeshaji (kujipatia kipato) hasa
ukizingatia kuwa wapo baadhi yetu tunaifanya kama ajira nyingine. Kimsingi
lazima tukubali kuwa mitandao hii imekuwa tegemeo kubwa la kusambaza habari
mbalimbali tena kwa muda mfupi tangu kutokea kwa tukio fulani, hivyo kuna kila
sababu ya kuendelea kuwapiga msasa wanaoiendesha ili kupunguza matumizi mabaya
ya mitandao hii.
TBN
inaamini njia pekee ya kupambana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ni
kuendelea kutoa elimu kwa waendeshaji na watumiaji ili mwisho wa siku
wasikubali kutumika vibaya au kuitumia vibaya mitandao hii katika kutoa
taarifa. Kwa dunia ya sasa hakuna atakayepinga kuwa mitandao hii imekuwa
ikielimisha umma, ikikosoa jamii na kiburudisha juu ya masuala anuai ya kijamii.
TBN
inapenda kutoa shukrani kwa Serikali ya Awamu ya Nne na Tano chini ya Mh. Rais
John Pombe Magufuli kwa ushirikiano alioanza kuuonesha hasa kwa kutambua
mchango wa mitandao hii ya kijamii na hata kuitumia katika utoaji wa taarifa
zao. Kimsingi hii ni hatua nzuri na ya kuigwa hasa katika ulimwengu huu ambapo
dunia imekuwa kama kijiji kutokana na hatua ya maendeleo ya habari na
mawasiliano.
Ndugu Wanahabari,
Kwa
kulitambua hili mnaweza kuona hata taasisi nyeti kama Ikulu nayo ina Blogu
maalumu kwa ajili ya kutoa taarifa kwa umma, Idara ya Habari Maelezo nayo ina
Blogu kwa ajili ya kutoa taarifa kwa umma juu ya masuala mbalimbali yanayopaswa
kutolewa kitaarifa kwa jamii. Jambo la kujivunia zaidi kwa maendeleo ya
mitandao hii hata Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh.
Nape M. Nnauye amekuwa mstari wa mbele kuona umuhimu wa mitandao ya kijamii
hasa blogu na hata kuzitumia katika kupasha habari umma. Hata katika mkutano
wetu wa kesho kutwa ndiye tunayemtarajia kuwa mgeni rasmi atakayetufungulia
mkutano huo.
Ndugu Wanahabari,
Kwa
namna ya pekee TBN inapenda kutoa shukrani za pekee kwa Benki ya NMB kwa
kukubali kuwa wadhamini wa kuu wa mkushanyiko huo wa 'bloggers' kutoka maeneo
mbalimbali ya mikoa yetu. Kitendo cha kujitolea kufanikisha jambo hili
kinaonesha namna gani NMB inavyowajali wananchi katika masuala mbalimbali
ikiwemo hili la upashanaji habari kwa jamii.
Kama
hiyo haitoshi tunapenda kuwashukuru wadhamini wengine ambao ni NHIF, SBL, PSPF
na Coca Cola ambao wamejitolea kuungana nasi katika kufanikisha tukio hili la
kuwaleta pamoja bloggers na kutoa mafunzo kwao. Tunaamini tutakuwa nao siku
zote katika masuala mengi ya maendeleo ya tasnia ya mitandao ya kijamii.
Imetolewa na; Mwenyekiti wa Muda wa TBN
Joachim E. Mushi
0756469470
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :