TAARIFA YA TANZANIA BLOGGERS NETWORK (TBN) KWA UMMA TAREHE 4/12/2016, DAR ES SALAAM.
Posted in
afrika mashariki
No comments
Sunday, December 4, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Chama cha Wamiliki/Waendeshaji wa Mitandao ya Kijamii nchini 'Tanzania Bloggers Network' (TBN) kilichosajiliwa rasmi na Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani, mwezi Aprili, 2015 na kupewa namba ya usajili, S. A 20008.
Kinapenda kuwataarifu kuwa kinatarajia kuanza mkutano wake mkuu na mafunzo kwa Bloggers kesho Jumatatu tarehe 5 -6 mwezi wa 12/2016.
Mkutano huo na mafunzo
kwa wanachama utafunguliwa rasmi na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO),
Dk. Hassan Abbas katika Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Golden Jubilee Tower
jijini Dar es Salaam. Mkutano huo uliodhaminiwa na Benki ya NMB na wadhamini
wengine unatarajia kuanza majira ya saa mbili na nusu asubuhi na kufanyika kwa
siku mbili mfululizo.
Katika mkutano huu wanatasnia
watapewa semina juu ya uendeshaji mitandao ya jamii kwa manufaa, upashaji
habari kwa kutumia mitandao yao kwa kuziangatia maadili na namna ya kunufaika
na mitandao hiyo kwa waendeshaji (kujipatia kipato) hasa ukizingatia kuwa wapo
baadhi yetu tunaifanya kazi hii kama ajira nyingine.
Aidha katika mkusanyiko
huu mbali na washiriki kupata mafunzo pia watapata muda wa kujadili masuala
mbalimbali ya umoja wao na kutoka na mkakati wa kuijenga zaidi TBN kwa
mafanikio ya wana Blogu.
Mkutano huu ni matokeo mazuri
ya ushirikiano kati ya TBN na wataalam wa masuala ya habari na mitandao ya
kijamii, ambao kwa pamoja tumeandaa semina hii kwa wanahabari wa mitandao ya
kijamii hasa 'Bloggers' kwa lengo la kujifunza zaidi na kujadili masuala
mbalimbali ya chama na tasnia nzima.
TBN inaendelea
kuishukuru Serikali kupitia taasisi zake ikiwemo Mamlaka ya Udhibiti Mawasiliano nchini (TCRA) kwa kutoa
ushirikiano mkubwa hadi kuwezesha chama hiki cha wamiliki/waendeshaji mitandao
ya jamii kukamilisha mchakato wa usajili wake.
Lakini kwa namna ya
pekee nayapongeza pia makampuni mengine yakiwemo PSPF, NHIF, SBL, na Coca Cola kwa
kuungana nasi katika kufanikisha tukio hili la kuwaleta pamoja bloggers kwa
lengo la kuwanoa zaidi juu ya shughuli wanazozifanya.
Kimsingi lazima tukubali
kuwa mitandao hii imekuwa tegemeo kubwa la vyanzo vya habari na kusambaza
taarifa mbalimbali tena kwa muda mfupi, hivyo kuna kila sababu ya kuendelea
kuwanoa wanaoiendesha ili kupunguza matumizi mabaya ya mitandao hii.
TBN inaamini njia pekee
ya kupambana na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ni kuendelea kutoa elimu
kwa waendeshaji na watumiaji ili mwisho wa siku wasikubali kutumika vibaya au
kuitumia vibaya mitandao hii katika kutoa taarifa. Kwa dunia ya sasa hakuna
atakayepinga kuwa mitandao hii imekuwa ikielimisha umma, ikikosoa jamii na
kiburudisha juu ya masuala anuai ya kijamii.
Imetolewa
na; Mwenyekiti wa Muda wa TBN
Joachim
E. Mushi
0756469470
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :