Mursi aapishwa mjini Cairo
Posted in
No comments
Saturday, June 30, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Kiongozi wa mwanzo wa Misri
aliyechaguliwa kwenye uchaguzi huru, Mohammed Morsi, amekuwa rais mpya
baada ya kuapishwa mbele ya mahakama ya katiba mjini Cairo.
Bwana Morsi kutoka chama cha Muslim
Brotherhood anakuwa rais wa mwanzo wa chama cha Kiislamu, na wa kwanza
ambaye hatoki katika jeshi.
Chama chake kilikuwa kimepigwa marufuku wakati wa utawala wa Rais Mubarak.
Ameahidi kuwalinda watu wa Misri, na kuheshimu katiba na sheria.
Jaji mmoja kwenye sherehe hiyo ya kuapishwa kwa rais, alisema leo ni siku kubwa kwa Misri, ukurasa mpya wa heshima na mafanikio.
Mwandishi wa BBC mjini Cairo anasema watu walishangaa kuona ulinzi ni mchache katika eneo la mahakama ya katiba, kuonesha kuwa Bwana Morsi anataka kuwa mtu wa watu.
Hapo jana, Bwana Morsi alikula kiapo cha alama tu, mbele ya mamia ya wafuasi wake katika medani ya Tahrir, mjini Cairo - chimbuko la mapinduzi yaliyomuondoa Rais Mubarak.
Lakini mwandishi wetu anasema, haijulikani jeshi litampa rais mpya kiwango gani cha madaraka.

Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :